Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto mmoja kati ya watoto 160 anakabiliwa na usonji: WHO

Mtoto mmoja kati ya watoto 160 anakabiliwa na usonji: WHO

Pakua

Usonji! Ni tatizo la kiafya ambalo linaelezwa kusumbua watoto duniani lakini mara nyingi ni vigumu wazazi au jamii kutambua. Watoto hutelekezwa kwa kuonekana pengine ni vichaa na kubandikwa majina ya kukatisha tamaakamavile laana! Aghalabu watoto hawa kufurahia maisha kwani jamii huwatenga na shuleni nako hukataliwa. Wazazi hukumbwa na mkwamo. Takwimu za shirika la afya duniani, WHO zinasema kuwa mtoto mmoja kati ya watoto 160 anakabiliwa na Usonji. Lakini Usonji ni nini hasa? Na nini kinafanyika kupatia suluhisho kwa watoto na familia zao? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii ya wiki.