Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha Gabriella na Autism Connects Tanzania waleta nuru kwa watoto wenye Usonji

Kituo cha Gabriella na Autism Connects Tanzania waleta nuru kwa watoto wenye Usonji

Pakua

Aprili Pili ni siku ya kimataifa ya Usonji. Dunia imekuja pamoja kwa ajili ya kuhamasisha jamii na kuelimisha kuhusu ugonjwa huo ambao mbali na changamoto ya huduma ya afya hususan katika mataifa yenye kipato cha chini, kuna pengo uelewa juu ya ulemavu wa akili au usonji. Katika mahojiano maalum na Idhaa hii Brenda Shuma, Mkurugenzi wa Kituo cha Gabriella kilichoko mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania alizungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu usonji au Autism kwa kingereza na hapa anaanza kwa kueleza dalili zinazodhihirika kwa mtu mwenye usonji.