Watoto warohigya waliosalia Myanmar wanaishi maisha dhalili- UNICEF
Kitendo cha kushindwa kuwafikia watoto wa kabila la Rohingya ambao bado wamesalia nchini Myanmar kinatutia shaka kubwa kwa kuwa wanaishi kwenye mazingira ya kusitikisha.
Kitendo cha kushindwa kuwafikia watoto wa kabila la Rohingya ambao bado wamesalia nchini Myanmar kinatutia shaka kubwa kwa kuwa wanaishi kwenye mazingira ya kusitikisha.
Nchini Zambia, shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM kwa kushirikiana na serikali wanajenga kituo cha kuhifadhi wahamiaji walio hatarini zaidi kwenye mpaka wa nchi hiyo na Namibia.
Maisha ya wakimbizi wa Syria waliokosaka hifadhi Lebanon yanazidi kuwa hatarini kila uchao, wakati huu ambapo zaidi ya nusu yao ni mafukara.
Hiyo ni kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la wakimbizi, UNHCR, la watoto, UNICEF na lile la mpango wa chakula WFP.
Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women kwa ushirikiano na Bank ya maendeleo Afrika ADB wameanzisha mpango wenye lengo la kuwakwamua wanawake barani Afrika kutoka kwenye umasikini
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mlipuko wa ugonjwa wa tauni nchini Madagascar unaweza kusalia historia iwapo mamlaka nchini humo zitakuwa na uwekezaji wa kimkakati.
Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa vyoo safi na salama ni hatarishi kwa afya ya binadamu.
Nchini Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali wamehitimisha kampeni ya siku tano ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua iliyolenga watoto milioni 4.2 nchini kote.
Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Halisi", “Uhalisi” na "Uhalisia". Mchambuzi wetu ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.
Umoja wa Mataifa umeshtushwa na taarifa kuwa ndani ya wiki moja watu 20 wamenyongwa hadi kufa huko nchini Misri baada ya kushtakiwa katika mahakama ya kijeshi nchini humo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mkutano wa wazi kuhusu hali inayoendelea nchini Iran, kufuatia maandamano yaliyofanyika nchini humo tangu tarehe 28 mwezi uliopita hadi Jumanne wiki hii.