Vyoo vinaokoa maisha, kinyesicho chenda wapi?:UM
Vyoo vinaokoa maisha kwa sababu kinyesi cha binadamu husambaza magonjwa yanayokatili maisha ya watu wengi.
Vyoo vinaokoa maisha kwa sababu kinyesi cha binadamu husambaza magonjwa yanayokatili maisha ya watu wengi.
Kwa mara ya tatu ndani ya siku mbili baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa limeshindwa kupitisha azimio la jukumu la jopo la kimataifa linalochunguza matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria kutokana kwa sababu ya kura ya turufu ya Urusi nchi ambayo ni mjumbe wa kudumu wa baraza hilo.
Fursa za kiuchumi na kijamii kwenye ukanda wa Mediteranea ambao kihistoria unatambulika kwa maendeleo ya kitamaduni, hivi sasa ziko mashakani kutokana na ukanda huo kughubikwa na matatizo.
Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Bwela Suti". Mchambuzi wetu ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.
Muziki wa asili umekuwa haupatiwi kipaumbele na vijana wengi maeneo mbali mbali duniani licha ya kuwa ni sehemu ya utamaduni wao kwani unazungumzia asili yao.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameonyesha hali ya wasiwasi juu ya kuwepo kwa uwazi na uhuru kwenye uchaguzi nchini Cambodia baada ya mahakama kuu nchini humo kufuta usajili wa chama kikuu cha upinzani kwa miaka mitano.
Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko la mauaji na vitisho dhidi ya watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa kijamii katika jimbo la pwani ya Pacific nchini Colombia ambapo wahanga katika visa vingi ni kutoka jamii za wa
Nishati ya jua imeleta nafuu katika utoaji wa huduma za afya kwenye wilaya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi warohingya kutoka Myanmar wamesaka hifadhi.
Juhudi za kimataifa za kupambana na kuenea kwa usugu wa vijiumbe maradhi mashambani na kwenye mfumo wa chakula zina shika kasi , kutokana na kuungwa mkono na serikali na msaada wa kiufundi unaoziwezesha nchi kukabili tatizo hilo limesema shirika la shakula na kilimo FAO hii leo.
Harakati za warohingya kukimbia nchi yao Myanmar kutokana na mateso zinazidi kutia wasiwasi zaidi wakati huu ambapo wanaendelea kumiminika Bangladesh kwa kutumia usafiri unaotishia zaidi maisha yao.