Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 JUNI 2024

26 JUNI 2024

Pakua

Hii leo jaridani Tunafuatilia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini Kenya, na ripoti ya utumiaji wa dawa za kulevya. Makala tunarejea nchini Kenya kufuatilia matibabu ya waathirika wa dawa za kulevya na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?

  1. Viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekazia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres kwa mamlaka za Kenya kufuatia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini humo Juni 18 kupingwa muswada wa fedha wa mwaka 2024.
  2. Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema leo Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC.
  3. Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na ulanguzi wa madawa hizo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa na Uhalifu (UNODC) wamechapisha ripoti yao inayosisitiza haki ya afya kwa wote ikiomba Umoja wa Mataifa kuongza kasi katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa. Kevin Keitany wa redio Washirika wetu Domus FM anatupeleka nchini Kenya kufuatilia juhudi za mashirika ya kiraia na serikali hasa katika huduma za afya kwa waathirika wa madawa ya kulevya na pombe.
  4. Mashinani tunaelekea nchini Sudan kusikia simulizi ya mwathirika wa vita inayoendelea nchini humo.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'58"