Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 JUNI 2024

24 JUNI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza hasa kwa watoto, na ziara maalum ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS. Makala inatupeleka nchini India na mashinani nchini Uganda, kulikoni? 

  1. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini, hii leo Juni 24 ametahadharisha vikali kwamba UNRWA itaporomoka kama ufadhili hautapatikana haraka, na "kizazi kizima" cha watoto wako katika hatari ya kuangukia kwenye "umaskini, chuki na migogoro ya baadaye”. 
  2. Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi..
  3. Katika makala Assumpta Massoi anatupeleka India kumulika jinsi mradi wa Benki ya DUnia umeondolea kaya adha ya changamoto za kiafya na kiuchumi zitokanazo na matumizi ya kuni na samadi ya ng'ombe kwenye kupikia.
  4. Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kusikia ujumbe wa kiongozi wa jamii ambaye ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
9'52"