Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yawaleta pamoja wadau wa AI na Filamu kujadili fursa na changamoto zinazowakabili

Utafiti wa Shirika la Kimataifa la Kazi umebaini kuwa kazi nyingi na viwanda vitakunufaika na Akili Mnemba lakini ajira kama za ukarani zitachukuliwa na Akili Mnemba kwa kiasi kikubwa.
© Unsplash/Steve Johnson
Utafiti wa Shirika la Kimataifa la Kazi umebaini kuwa kazi nyingi na viwanda vitakunufaika na Akili Mnemba lakini ajira kama za ukarani zitachukuliwa na Akili Mnemba kwa kiasi kikubwa.

UNESCO yawaleta pamoja wadau wa AI na Filamu kujadili fursa na changamoto zinazowakabili

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Akili mnemba (AI) imebadili fani ya sanaa na utamaduni kwa njia ambazo haikutarajiwa. Hata hivyo mabadiliko hayo ni ya muda mrefu. Ili kuwapa Jukwaa wataalam wa Sanaa na dijitali, shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mkutano maalum ili kujadili athari za akili mnemba kwenye sekta ya filamu.

Mkutano huo umewaleta pamoja huko jijini Paris Ufaransa, wataalamu wa masuala ya AI na filamu kutoka kila pembe ya dunia ambao wamejadiliana manufaa na changamoto ziletwazo na maendeleo ya akili mnembo katika sekta za utamaduni na sanaa ukizingatia maadili na ubunifu.

Kwa pamoja, wataalamu hayo wa sekta hizo mbili zinazokuwa kwa kasi katika ulimwengu wa teknolojia wameshirikishana maarifa na kubadilishana mitazamo kuhusu mazingira ya sasa ya AI katika sekta ya filamu na kuzingatia hatua zinazofuata na ulinzi wa kazi zao.

Kwa muda mrefu sekta za ubunifu imekuwa mstari wa mbele katika kujieleza pamoja na uvumbuzi, wasanii wamesaidia kuielimisha jamii kwa kutoa changamoto kwenye mila destuli wa kanuni za jamii husika.

Mkutano huu muhimu umekuja muda muafaka ikizingatiwa migomo ya hivi karibuni ya waandishi na waigizaji huko nchini Marekani ambao walieleza wasiwasi wao kuhusu uwazi, haki miliki na malipo ya haki ya kazi zao katika muktadha wa AI pamoja na athari zinazoonekana na mabadiliko ya kielektroniki katika filamu na sekta nyinginezo za kitamaduni na ubunifu.

Hata hivyo watetezi wa AI wanaona maendeleo hayo ni fursa ya kuimarisha ubunifu kwa kutoa zana na njia mpya za msukumo na ushirikiano, na kwa demokrasia hususan katika makundi yasiyo na uwakilishi.