Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku 100 kuelekea Siku ya Kimataifa ya Amani tupande mbegu za haki na matumaini - Guterres

Njiwa wa amani wakipaa angani katika viwanja vya msikiti wa kihistoria wa Hazrat-i-Ali, katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan. (Maktaba)
UN Photo/Helena Mulkerns
Njiwa wa amani wakipaa angani katika viwanja vya msikiti wa kihistoria wa Hazrat-i-Ali, katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan. (Maktaba)

Siku 100 kuelekea Siku ya Kimataifa ya Amani tupande mbegu za haki na matumaini - Guterres

Amani na Usalama

Zikiwa zimesalia siku 100 kamili kufika Septemba 21 tarehe ambayo kila mwaka huadhimishwa Siku ya Kimataifa ya Amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza, “mazungumzo, huruma na haki za binadamu kwa wote.”

Kupitia ujumbe mfupi wa maandishi uliosambazwa leo Juni 13, Guterres anasema, “Katika ulimwengu uliojawa na migogoro, ukosefu wa usawa na ubaguzi, lazima tujitahidi zaidi kukuza mazungumzo, huruma na haki za binadamu kwa wote.”
 
Kila mwaka ifikapo tarehe 21 Septemba, Umoja wa Mataifa hualika ulimwengu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani. Lengo la mwaka huu ni "Kukuza utamaduni wa amani".
 
Bwaa Guterres anasisitiza akisema, “Tunapoanza kuhesabu siku 100 kuelekea Siku ya Amani, hebu tupande mbegu za haki na matumaini na kutokuwa na vurugu.”
 
Siku ya Kimataifa ya Amani ilianzishwa mwaka 1981 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Miongo miwili baadaye, mwaka wa 2001, Baraza Kuu lilipiga kura kwa kauli moja kuteua Siku hiyo kama kipindi cha kutofanya vurugu na kusitisha mapigano.