Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira ambayo mamlaka ya Israel inawashikilia Wagaza yanatia hofu kubwa: UN

Sehemu kubwa ya Khan Younis imesalia magofu.
© UNOCHA/Themba Linden
Sehemu kubwa ya Khan Younis imesalia magofu.

Mazingira ambayo mamlaka ya Israel inawashikilia Wagaza yanatia hofu kubwa: UN

Amani na Usalama

Huku kukiwa na ripoti zaidi za mashambulio ya mabomu huko Gaza usiku wa kuamkia leo Jumanne, Umoja wa Mataifa na mashirika wadau wameelezea wasiwasi wao juu ya hali ya kikatili isiyo ya kibinadamu wanakoshikiliwa na mamlaka ya Israel washukiwa wa wapiganaji wa Kipalestina katika eneo la makazi “kukiwa na madai ya unyanyasaji dhidi yao kiasi kwamba wengine walilazimika kukatwa miguu kutokana na kufungwa pingu kwa muda mrefu”.

Katika ripoti mpya iliyotolewa juu ya hali ya Gaza kwa mwezi Mei 2024, waandishi wa ripoti wameelezea ushuhuda walioupata kutoka kwa madaktari na wavuja taarifa" kwamba wafungwa waliojeruhiwa wameshikiliwa katika hospitali ya shamba huku wakiwa na pingu na minyororo miguuni na kufungwa macho na kwa vitambaa kwa saa 24 siku s7 za wiki katika vitanda vyao".

Hofu ya mateka

Aidha, waandishi wa ripoti hiyo wamesema hadi kufikia tarehe 19 Mei, watu 128 kati ya 253 waliotekwa wakati wa mashambulizi ya kigaidi yaliyoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana bado wamesalia Gaza, wakisisitiza kwamba kuchukuliwa kwa mateka ni "uvunjaji mkubwa wa mikataba ya Geneva ya uhalifu wa kivita." 

Zaidi ya mateka 35 wametangazwa kuwa wamekufa na wale ambao bado wako hai wanaweza kukabiliwa na "hali mbaya zaidi", huku maelezo kutoka kwa wale walioachiliwa yakionyesha "ripoti nyingi za unyanyasaji wa kijinsia wakiwa utumwani".

Wanawake wazee walikimbia Khan Younis, baada ya jeshi la Israeli kushambulia mji huo.
© UNOCHA/Ismael Abu Dayyah
Wanawake wazee walikimbia Khan Younis, baada ya jeshi la Israeli kushambulia mji huo.

Kambi ya jangwani

Tukirejea kwa wafungwa wa Kipalestina, shuhuda zinaonyesha kwamba wafungwa "wanalishwa kwa kutumia majani, na kesi kadhaa za wafungwa kukatwa viungo vyao kutokana na kufungwa pingu kwa muda mrefu", kulingana na taarifa kutoka kwa Global Protection Cluster, ambayo inaleta pamoja mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika mengine ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Taarifa hiyo inaangazia wasiwasi wa awali kuhusu madai ya unyanyasaji wa wafungwa kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR na wataalam huru wa haki lakini jeshi la Israel hapo awali limekanusha madai hayo.

Takriban wafungwa 27 kutoka Gaza inaaminika wana uwezekano wa kufa wakiwa kizuizini katika kambi ya jeshi ya Israel ikiwa ni pamoja na Sde Teiman katika jangwa la Negev nchini Israel, huku wengine "angalau wanne kutoka katika kizuizi hicho walikufa katika vituo vya Jeshi la Magereza la Israel (IPS) ama kwa sababu. ya madai ya kupigwa au kukosa msaada wa matibabu.”

Shambulio la Israel Mei 26 lilipiga kambi ya wakimbizi wa ndani Rafah
UNRWA
Shambulio la Israel Mei 26 lilipiga kambi ya wakimbizi wa ndani Rafah

Kufungwa macho na kufungwa pingu

"Iwe wanazuiliwa katika vituo vya IPS au vya kijeshi, wafungwa wanaripotiwa kukabiliwa na hali ngumu sana ya kuwekwa kizuizini, ikiwa ni pamoja na msongamano wa watu na wengine kuzuiliwa katika vituo vinavyofanana na ngome, wafungwa macho kila mara na kufungwa pingu mikononi, kukosa fursa ya kwenda mmsalani, kuathiriwa na ukosefu wa vifaa, utoaji wa chakula na maji kwa wingi hautoshi kuishi.”

Wanawake na watoto ni miongoni mwa wale wanaoshikiliwa walikamtwa wakati wa kamatakamata ya watu wengi iliyofanywa na jeshi la ulinzi la Israeli, ripoti hiyo imeendelea kusema, ikiongeza kuwa familia nyingi "hazina taarifa kuhusu wapendwa wao, wakati Israeli inashindwa au inakataa kutoa habari juu ya mahali walipo au hatima ya wengi wa wale waliowekwa kizuizin. Wavulana wenye umri wa miaka 14 na zaidi kwa kawaida huzuiliwa na wanaume watu wazima. Watoto wadogo wanazuiliwa na wanawake na wanafamilia wazee, kwa kawaida huwa ni kwa muda mfupi zaidi.”

Takriban watu 810.000 wamekimbia Rafah katika wiki chache zilizopita
© UNRWA
Takriban watu 810.000 wamekimbia Rafah katika wiki chache zilizopita

Kukamatwa kwa watu wengi

Jeshi la Israel hivi karibuni limedai kuwazuia Wapalestina 2,300 kutoka Gaza wakati wa operesheni za ardhini huko Gaza, waandishi wa ripoti hiyo wamesema, na kuongeza kwamba idadi halisi ilikuwa kubwa zaidi.

Mwishoni mwa Aprili, takriban wafungwa 865 walishikiliwa kama "wapiganaji kinyume cha sheria", aina isiyojulikana chini ya sheria za kimataifa. 

Shuhuda nyingi zenye kuhuzunisha zaidi zinaonyesha kwamba wafungwa wanakabiliana na kulazimishwa kukaa utupu bila nguo, kunyanyaswa kingono, vitisho vya kubakwa, na vilevile kuteswa kupitia vipigo vikali, kushambuliwa na mbwa, kupekuliwa ndani ya nguo zao, kuzamishwa katika maji, na kunyimwa chakula, usingizi, na kunkataliwa kwenda msalani miongoni mwa vitendo vingine vya kikatili”.

Kulingana na maelezo kutoka kwa wafungwa walioachiliwa na wahudumu wa matabibu wanaoweza kuwafikia wale wanaozuiliwa, lengo la matibabu haya ni kuibua maungamo ya kulazimishwa na uchunguzi kwa watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa vikundi vyenye silaha vya Palestina.