Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tarajieni joto kali katika miezi ijayo:WMO

Jioni ya majira ya joto katika kitongoji cha Smolensk, mjini Dorogobuzh nchini Urusi
Picha na WMO/Alexey Sergovantsev
Jioni ya majira ya joto katika kitongoji cha Smolensk, mjini Dorogobuzh nchini Urusi

Tarajieni joto kali katika miezi ijayo:WMO

Masuala ya UM

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO leo limetoa tahadhari kwamba joto la kupita viwango vya wastani litarajiwe kwenye sehemu nyingi duniani katika miezi michache ijayo hata kama hakutokuwepo na matukio ya El Niño.

Shirika hilo la WMo limesema kwamba kuna uwezekano wa asilimia 60 wa kuendelea na hali inayoweza kusababisha El Niño kwa mwezi Machi na Mei 2020, lakini uwezekano wa kutokea El Niño ni asilimia 35 au La Niña ni asilimia 5.

Na kwa mwezi June hadi Agosti 2020 uwezekano wa El Niño ni asilimia 20-25% na La Niña pia ni asilimia 20-25%.

Taarifa mpya za hali ya hewa duniani zinasema joto la viwango vya zaidi ya wastan zinatarajiwa katika sehemu kubwa ya dunia kote katika maeneo ya tropiki na kwenye ukame zaidi.

Na matokeo yake WMO inasema kati ya mwezi Machi hadi Mei 2020 inaashiria kutakuwa na joto la kupita kiwango cha wastani hususan katika maeneo ya Kitropiki. Viwango vya juu wa hali ya kawaida ya hewa vinatarajiwa kaskazini mwa Ikweta katikati ya maeneo ya kitropiki ya Pasifiki na na Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi hadi Mashariki mwa Afrika Mashariki kwenye eneo la ikweta.

Pia hali inatarajiwa kuwa tofauti katika maeneo ya Amerika Kusini, Amerika ya Kati, Caribbea na Kusini mwa afrika kwa mujibu wa makadirio ya utabiri wa hali ya hewa wa WMO.

Shirika hilo limeongeza kuwa maeneo ya Kusini Mashariki mwa Asia, Ocenia na Magharibi mwa Australia pamoja na Kusini mwa afrika, Amerika ya Kati na Caribbea yalishuhudia hali kame zaidi ya kawaida kwa miezi ya Novemba na Januari.