Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nika Alexander: Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha

Daktari akimtibu mgonjwa mdogo katika hospitali ya Al-Aqsa katikati mwa Gaza. (Maktaba)
WHO
Daktari akimtibu mgonjwa mdogo katika hospitali ya Al-Aqsa katikati mwa Gaza. (Maktaba)

Nika Alexander: Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha

Amani na Usalama

Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”

Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza tofauti ya kwanza anayoona sasa akiwa amerejea kutoka Gaza ambapo wakati angali kule siku baada ya siku wakisikia mlio wa ndege basi bomu linaweza kuanguka dakika yoyote, wakati sasa ukiwa sehemu ambayo si ya vita akisikia mlio wa ndege pengine ni watu wanaendea likizo ni kama watu wa Gaza wanaishi kinyume na ulimwengu. 

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kurejea Gaza Bi.Nika anasimulia hali ya kule. 

“Nilichoondoka nacho ni mawazo ya jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu wa Gaza, jinsi hali ilivyo ngumu kwa watu wanaojaribu kuwasaidia watu wa Gaza na jinsi kulivyo hatari.” 

Amesema hospitali zinazofanya kazi ni chache na hazifanyi kazi kamili.

“Kimsingi, kote Gaza, ni theluthi moja ya hospitali ndio zinafanya kazi. Kwa hivyo takriban hospitali 12 kati ya 36 bado zinaweza kufanya kazi kwa namna fulani. Hawawezi kutoa huduma kamili. Baadhi yao wanafanya kama sehemu ya kutoa huduma ya kwanza na kusaidia wenye kiwewe, ambapo wanajaribu tu kutibu wake wanakuwa wanavuja damu na vyovyote vile wawezavyo ilimradi watu wasife kutokana na majeraha.”

Afisa huyu wa mawasiliano ya dharura anasema pamoja na yote hayo lakini lipo lililompa matumaini licha ya kutokuwepo kwa eneo lolote salama katika Ukanda wa Gaza. 

“Kilichonivutia sana ni kwa jinsi kila mtu anavyofanya kazi kwa bidii licha ya hali mbaya ambapo kila kelele inaweza kuwa ni mlipuko karibu yako, au unaweza kuwa unakulipukia wewe. Nilipoondoka Rafah wiki moja iliyopita, tulikuwa wafanyakazi 19 wanaondoka na wengine 20 wa Umoja wa Mataifa wanaingia Rafah. Ninawaona wenzangu hao kuwa wajasiri sana, na sio kwamba wanakuja kujifanyia kazi wenyewe bali wanakuja kushirikiana na wafanyakazi wa Gaza wa sekta ya afya.”