Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji sio tu ni uhai bali ni muhimu wa kila kitu: Guterres

Wanakijiji wa Zambia wanapata maji safi kutoka kwa kisima cha jumuiya.
© UNICEF/Kinny Siakachoma/OutSe
Wanakijiji wa Zambia wanapata maji safi kutoka kwa kisima cha jumuiya.

Maji sio tu ni uhai bali ni muhimu wa kila kitu: Guterres

Tabianchi na mazingira

Jukwaa la 10 la maji duniani linaendelea Bali nchini Indonesia mwaka huu likimulima mwasuala sita muhimu ambayo ni 

  • Uhakika wa maji na ustawi
  • Maji kwa ajili ya binadamu na asili
  • Kupunguza na kudhibiti hatari za maafa
  • Utawala, ushirikiano na diplomasia ya maji
  • Ufadhili endelevu wamaji
  • Maarifa na ubunifu

Katika ujumbe wa video Kwenye Jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameishukuru seriiali ya Indonesia na Baraza la Maji Duniani kwa kuangaa jukwaa hilo huku akisisitiza kwamba “Maji ni uhai. Ni muhimu kwa watu wenye afya nzuri, mifumo ya ikolojia na bayoanuwai."

Ameongeza kuwa “Na kama mada ya mwaka huu inavyotukumbusha, maji ni ufunguo wa ustawi wetu wa pamoja. Hata hivyo maji yako katika tishio kubwa, ushindani usio na maana, utumiaji usio na akili na uchafuzi wa mazingira usiojali unamaliza na kutia sumu damu ya maisha ya ulimwengu.”

Mabadiliko ya tabianchi ni sumu ya maji

Katibu Mkuu ameongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi yanasukuma joto la maji hadi viwango vipya vya hatari.

Barafu inayeyuka, bahari inaongezeka, na mtiririko wa mito unapungua.

Amesisitiza kuwa na “Na watu ndio wanaolipa gharama kubwa katika ukame, mazao yao yaliyoharibiwa, utapiamlo, magonjwa na majanga.”

Na anasema Serikali kote ulimwenguni zinaamka kwa kwenye janga hii.

Jukwaa hili ni fursa muhimu

Katibu Mkuu amresema ’’Jukwaa hili ni fursa muhimu ya kujadili suluhu kuhusu maji na usafi wa mazingira, kupunguza hatari za maafa, utawala bora, fedha na uvumbuzi. Umoja wa Mataifa unasimama nanyi katika juhudi hizi.”

Kufuatia Mkutano wa Maji wa Umoja wa Mataifa wa mwaka jana, Guterres amesema ’’mkakati wa mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji na usafi wa mazingira mwezi Julai.’’

Amekumbusha kuwa mikutano ya maji ya Umoja wa Mataifa mwaka 2026 na 2028 itakuwa nyakati muhimu kwa ulimwengu kusongesha kazi hii mbele.

Ameiihimiza dunia kwamba ‘’Tunahitaji kuweka maji katikati ya juhudi zetu zote juu ya hali ya hewa, viumbe hai na maendeleo endelevu. Hebu tufanye kazi kama kwa pamoja ili kulipa suala hili muhimu umakini unaohitajika. Tuchukue hatua kwa ajili ya maji.’’

Kinachotarajiwakatika jukwaa hilo

Katika jukwaa hilo la 10 la maji lilianza mwishoni mwa wiki 18 Mei na kutarajiwa kufunga pazia 25 Mei  kinachotarajiwa ni ’’Hatua za kutekelezwa katika ngazi mbalimbali za kisiasa ambazo ni hatua za sera, suluhu, mipango ya utekelezaji na ahadi

Za uhamasishaji wa wadau wa umma na binafsi kutoka ndani na nje ya jumuiya ya maji.’’ 

Pia uundaji wa mbinu zinazoonekana za kiufundi, kulingana na sera na mikakati ya vitendo ya kufanya mipango kuundwa na kutekelezwa wasuluhu hizo.