Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzigo wa madeni unapora maendeleo ya mataifa mengi:Guterres

Katibu Mkuu Antonio Guterres akizungumza katika mkutano wa kamati ya maendeleo ya IMF mjini Bali, Indonesia
Grant Ellis / World Bank
Katibu Mkuu Antonio Guterres akizungumza katika mkutano wa kamati ya maendeleo ya IMF mjini Bali, Indonesia

Mzigo wa madeni unapora maendeleo ya mataifa mengi:Guterres

Ukuaji wa Kiuchumi

Mzigo mkubwa wa madeni kwa mataifa mengi unazuia maendeleo ya kiuchumi ya mataifa hayo pamoja na kuchukua raslimali nyingizinazohitajika  ili kuweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs.

Tahadhari hiyo limetolewa  leo Jumamosi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, mjini Bali, Indonesia wakati akihutubia mkutano wa kamati ya fedha ya shirika la fedha duniani IMFC ambao unahudhuriwa na  mawaziri wa fedha  pamoja na magavana wa benki kuu kutoka nchi mbalimbali, mkutano ulioandaliwa na shirika la fedha duniani IMF.

Katibu Mkuu, ametoa wito wa kuongezauwekezaji wa mda mrefu utakao leta tija duniani na kuweza kuondoa changamoto  katika ukuaji wa mazingira endelevu ya ujumuishwaji, na uthabiti wa uchumi.

Ameongeza kuwa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 yenye malengo 17 inatoa muongozo kwa ajili ya mwelekeo huo.

Hata hivyo amesema, ”tunajua kuwa changamotoni nyingi kama vile mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la kutokuwa na usawa, ukuaji wa mijina mengine.”

Katika muktadha huo  Guterres ametaja umuhimu wa kutekeleza  ajenda tekelezi ya Addis Ababa na kutaka  mkakati wake wa ajenda ya 2030 kuungwa mkono kifedha.

Ameeleza kuwa mkakati huo una vipaumbele vitatu tekelezi:será za kifedha na kiuchumi za ajenda ya 2030 ufadhili endelevu wa kitaifa na kikanda ilikuwawezesha vijana na wanawake kupata msaada wa kifedha.

Katibu Mkuu amesema kuwa  wizara za fedha pamoja na benki kuu ni muhimu katika maeneo yote, akihimiza kuwa wakishirikiana wataweza kuongoza sera zinazoitajikakuweka sawa masuala ya fedha.

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa unaweza kukomesha mifumo mibovu kama vile ya utoroshaji wa mitaji, pamoja na kukwepa kodi ambayo hufilisi mali asili za mataifa yanayoendelea.