Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani, Indonesia, Afrika Kusini, miongoni mwa wajumbe wapya baraza la Usalama

Wafanyakazi wa UN wakiwa wamebeba masanduku yenye kura wakati wa uchaguzi wa wajumbe watano wasio wa Kudumu wa Baraza la usalama.
Picha na UN/ Manuel Elias.
Wafanyakazi wa UN wakiwa wamebeba masanduku yenye kura wakati wa uchaguzi wa wajumbe watano wasio wa Kudumu wa Baraza la usalama.

Ujerumani, Indonesia, Afrika Kusini, miongoni mwa wajumbe wapya baraza la Usalama

Amani na Usalama

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa limewachagua wajumbe watano wapya wa baraza la usalama wasio wa kudumu.

Wajumbe hao waliochaguliwa kwa kura ya duru moja tu, kila mmoja atahudumu kwa kipindi cha miaka miwli kwenye baraza la usalama ambalo lina jukumu la kupanga ajenda nzima ya amani na usalama ya umoja wa Mataifa.

Nchini hizo Ujerumani, Indonesia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Dominica, na Ubelgiji watashikilia viti vya ujumbe huo kuanzia tarehe Mosi Januari mwaka 2019.

Wajumbe hao wapya watajaza nafasi zitakazoachwa wazi mwishoni mwa mwaka huu na Bolivia, Ethiopia, Kazakhstan, Uholanzi na Sweden  ambazo zote zimehudumu kwa miaka miwili kila moja miongoni mwa wajumbe 15 wa bazara hilo ambalo lina wajumbe watano tu wa kudumu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa , baraza la usalama jukumu lake kubwa ni kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa na nchi zote wanachama wanahitahjika kutimiza maamuzi ya baraza hilo.

Kikao cha Baraza la Usalama
UN /Mark Garten
Kikao cha Baraza la Usalama

 

Viti 10 vya ujumbe usio wa kudumu kwenye baraza la usalama vinagawanywa kwa kufuata mfumo wa mzunguko uliowekwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1963,  ili kuhakikisha usawa wa uwakilishi wa kikanda katika baraza hilo ambapo mgawanyo huo huwa ni: viti vitano kwa wajumbe kutoka Afrika, Asia na mataifa ya Pacific , kiti kimoja cha mjumbe kutoka Ulaya Mashariki, viti viwili wajumbe kutoka mataifa ya Amerika ya Kusini , na viti viwili wajumbe kutoka Ulaya Magharibi na mataifa mengine (WEOG).

Ubelgiji, na Ujerumani na Jamhuri ya Dominica na Afrika Kusini walipita bila kupingwa kutoka kwenye makundi ya kanda zao, wakati Indonesia ilijinyakuliwa kiti hicho baada ya duru ya pili ya mchuano na Moldives kuwania kidi cha kundi la asia-Pacific.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Dominica kuwa mjumbe asiye wa kudumu kwenye baraza la usalama . Na viti vitano vya kudumu kwenye baraza la usalama vinakaliwa na China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani.