Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MAHOJIANO: Matumaini yaongezeka kwa UN kuijaza Gaza kwa chakula, licha ya hofu ya uvamizi wa Rafah

Uharibifu mkubwa wa makazi ya watu Gaza
UN News/Ziad Taleb
Uharibifu mkubwa wa makazi ya watu Gaza

MAHOJIANO: Matumaini yaongezeka kwa UN kuijaza Gaza kwa chakula, licha ya hofu ya uvamizi wa Rafah

Msaada wa Kibinadamu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Gaza unaotaka kutalifurika eneo hilo kwa chakula na kuzuia njaa, umesonga mbele wiki hii kutokana na ahadi ya umma wa Israeli ya kuongeza mtiririko wa misaada, licha ya ishara ya leo Jumapili kwamba uvamizi unaohofiwa wa Rafah unakaribia.

Hayo ni kwa mujibu wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick, akizungumza kwa kina na UN News leo ikiwa ni miezi sita kamili tangu uhasama uanze kutokana na shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas Oktoba 7 mwaka jana.

Amesisitiza kwamba juhudi zote za misaada za Umoja wa Mataifa zinahusu kuokoa maisha na sio kitu kingine chochote.

Mkongwe huyo wa masuala ya kibinadamu ameyasema hayo wakati jeshi la ulinzi la Israel leo lilisema limeondoa baadhi ya vikosi vya wanajeshi kutoka Gaza ili kujiandaa kwa operesheni zijazo mwishoni mwa wiki wakati uongozi wa Israeli pia uliahidi kuongeza kiwango na mtiririko wa misaada kufuatia shinikizo kutoka ikulu ya Marekani Washington ingawa haijulikani ni lini mabadiliko yoyote katika sera yatatokea.

Bwana. McGoldrick amesema mchanganyiko wa shinikizo la kisiasa na la ndani na kuongezeka kwa lawama za kimataifa kufuatia mauaji ya wafanyakazi saba wa shirika la misaada la World Central Kitchen pamoja na miezi ya maombi ya Umoja wa Mataifa, inapaswa kutafsiri katika kuongeza msaada kwa Wagaza waliokata tamaa.

"Polepole lakini kwa hakika Waisraeli wanatambua ukubwa wa mgogoro wa kibinadamu, hasa kaskazini mwa Gaza. Tunatumai njia zote hizi zikifunguliwa tunaweza kuanza kuingiza na kujaza mahali hapo kwa chakula na vitu vingine, tunaweza kujitayarisha na chochote kinachofuata,”amesema.

Jamie McGoldrick Mratibu wa misaada ya kibinadamu katikia eneo la Palestina linalokaliwa akiwa Rafah Gaza Kusini
OHCA/oPt
Jamie McGoldrick Mratibu wa misaada ya kibinadamu katikia eneo la Palestina linalokaliwa akiwa Rafah Gaza Kusini

UN News: Itabidi tuanze na ripoti zinazoibuka kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka kusini mwa Gaza. Nini maoni yako kuhusu hilo?

Jamie McGoldrick: Nadhani awamu hii ya operesheni ya kijeshi, lazima wawe wamemaliza huko Khan Younis. Nadhani hapo ndipo wanatoa vikosi. Maana yake ni kwamba kwa matumaini hiyo itakuwa salama zaidi katika maeneo hayo na pengine watu wanaweza kuanza kurudi walikotoka. Lakini pia ni suala linalotia wasiwasi kwa maana kwamba labda wanatoka kujipanga upya na kujiweka tayari kwa uvamizi uliopendekezwa wa Rafah.

UN News: Umetaja kuwa Israel imejitolea kadha wa kadha kuongeza misaada kwa Gaza katika kujibu pia maombi ya mara kwa mara ya Umoja wa Mataifa. Umesema ahadi saba. Tafadhali unaweza kutufafanulia zilizo muhimu zaidi kati ya hizo?

Jamie McGoldrick: "Ndio, nadhani kwamba jambo muhimu zaidi kati ya hizo ni kupata fursa nyingi zaidi na njia zaidi kuingia Gaza. Ninamaanisha, hivi sasa tumewekewa vikwazo sana kwa kile tunachoweza kuleta.”

Tunayo sehemu kuu moja tu ya kuvuka, ambayo ni Kerem Shalom, hadi Rafah, na hiyo hutuwezesha kuingiza malori 250 kwa siku. Tunahitaji kupata hadi 500 pamoja na siku. Na ili kufanya hivyo tumekuwa tukiuliza tangu siku ya kwanza kwa vivuko zaidi kupitia kwenye kivuko cha Jordan hivi sasa, tunapata malori 100 pekee kwa wiki.

WAtoto wakijaza maji ya kunywa kwenye madumu huko kitongoji cha Al-Shaboura, eneo la Rafah, kusini mwa Gaza
UN News/Ziad Taleb
WAtoto wakijaza maji ya kunywa kwenye madumu huko kitongoji cha Al-Shaboura, eneo la Rafah, kusini mwa Gaza

Tunapaswa kuwa tunapata malori 30 hadi 50 kwa siku. Na kisha huko kaskazini, Ashdodi, bandari ya kisasa inayofanya kazi vizuri sana, tunaomba hiyo ifunguliwe tena. Na hilo linaweza kutuletea tena mlori mengine 100 kwa siku.

Kwa hivyo hivyo vivuko vikijumuishwa na Kerem Shalom, tungekuwa na takriban mlori 500 kwa siku, ambayo yangekidhi mahitaji ya Gaza. Na muhimu zaidi, kaskazini, ambapo kuna njaa inayokaribia haraka.

UN News: Katika mawasiliano yako na upande wa Israeli. Ahadi hizi zitatekelezwa lini, na unadhani watu wa Gaza wataanza kuhisi matumaini hayo lini?

Jamie McGoldrick: Kweli, tunatumai itakuwa haraka. Tuliambiwa, katika mikutano yetu ya Ijumaa, kwamba mambo haya yalikuwa yakiendelea na maandalizi yalikuwa yakifanyika. Na tunajua kulikuwa na mkutano jana huko Jordan na pande zote, Marekani, Umoja wa Mataifa na Jeshi la Jordan, ili kuja na njia fulani ya kushughulikia wigo mdogo tulio nao sasa.

Vile vile, tunasukumana na Waisraeli ili kujua ni lini tunaweza kupata bandari ya Ashdodi kufunguliwa kwa ajili ya vifaa zaidi na moja kwa moja hadi Erez, au mojawapo ya vivuko vingine vya kaskazini, bila kulazimika kuja kusini.

Nafikiri hilo litaruhusu ongezeko kubwa na la haraka la chakula kinachoingia. Kwa sasa, tunapata malori 10 hadi 20 pekee kwa siku fulani kuelekea kaskazini, na tunahitaji kuwa na malori 30 kila siku bila kukosa, ili tuweze kushughulikia uhaba mkubwa wa chakula na haswa njaa inayokuja miongoni mwa vikundi vilivyo hatarini zaidi huko.

Hospitali ya Kimataifa ya Kikosi cha Medical Corps huko Rafah, Gaza
WFP
Hospitali ya Kimataifa ya Kikosi cha Medical Corps huko Rafah, Gaza

UN News: Ahadi hizo zinatofautiana kutoka kwenye mipango hadi dhamira, je, zinatosha kutekeleza kiwango kikubwa ambacho Umoja wa Mataifa umetoa wito wa utoaji wa misaada na pia kuepusha njaa inayonyemelea Gaza?

Jamie McGoldrick: Hapana, nadhani tulichonacho mezani ni maendeleo haya ambayo tumeahidiwa. Na kama unavyokumbuka, walitoka nyuma ya kampeni ndefu ya utetezi sisi wenyewe na timu ya nchi kushinikiza fursa hizi, kushinikiza uingizaji msaada mkubwa zaidi, kusukuma utatuzi bora na ushirikiano bora na jeshi la IDF.

Na cha kusikitisha ni kwamba, hiyo imekuja tu kutokana na tukio kubwa sana lililotokea juzi la kuuawa kwa watu saba wa World Central Kitchen na pia kisiasa msukumo wa Rais Biden na simu kwa Waziri Mkuu Netanyahu.

Nadhani wale wote kwa pamoja karibu wakati huo huo katika wiki hii moja, na kisha kuruhusiwa kwetu sisi kisha kuanza kupata baadhi ya haya, tuseme, baadhi ya makubaliano haya tumekuwa tukiyauliza kwa muda.

Na nadhani kuna maana hapo na labda umuhimu hapo ambao hatupaswi kutarajia vyote kutokea mara moja, lakini tunaweza kuanza kuyafanyia kazi.

Lakini muhimu zaidi, tamko la umma linaturuhusu kuyakumbatia, na kisha tunaweza kurudi na kuyasukuma. Na hivi sasa tuna wajumbe wa ngazi za juu katika eneo hili na pia Tel Aviv, ambao wanajizatiti kwa masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na ahadi hizi zote mpya au makubaliano ambayo tumepewa.

Mtoto amesimama kwenye vifusi vya nyumba yake huko Gaza.
© Ziad Taleb
Mtoto amesimama kwenye vifusi vya nyumba yake huko Gaza.

UN News: Umesema kuwa Israel katika siku za hivi karibuni imekiri ukubwa wa mateso huko Gaza na uwezo wake wa kuwezesha ongezeko la misaada. Je, hiyo ni hoja nyingine kwamba Umoja wa Mataifa kweli ulikuwa umesimama tayari kufanya kila uwezalo lakini kulikuwa na vikwazo vingi? Na katika tathmini yako hiyo haikuwa wazi kwa mamlaka ya Israeli kabla ya mateso makubwa na uwezo wake wa kuyawezesha?

Jamie McGoldrick: Nadhani unapaswa kutambua kwamba kuna zaidi ya Israeli moja. Namaanisha, kuna, upande wa kisiasa wa mambo, ambao unaegemea sana mrengo wa kulia sasa.

Pia kuna baraza la mawaziri la vita linaloundwa na watu ambao wana malengo makubwa ya vita baada ya matukio ya kutisha ya tarehe 7 Oktoba. Halafu una mashirika ya kiraia ambayo yanasukuma sana mateka kuachiliwa.

Na hiyo ni sehemu ya pamoja ya jumuiya ya kiraia ya Israel na wanasiasa. Halafu una jeshi, jeshi lenyewe, IDF, tuna usimamizi wa uratibu wa mawasiliano, na tuna COGAT, ambayo ni chombo tunachoshughulikia mara kwa mara. Kwa hivyo kuna sehemu nyingi zilizogawanyika.

Na kwa hivyo, tunapaswa kutafuta njia ya kuwashawishi au kuwafanya waelewe. Na polepole lakini hakika hilo limetokea. Na nadhani linakuja kama matokeo ya moja kwa moja ya ushahidi kwamba tumeonyesha kuwa watoto zaidi kuliko inavyopaswa kuwa, wamekufa kaskazini kwa utapiamlo na kupungua uzito.

Wanapaswa kuelewa ni kwa nini tuko pale na kile tunachojaribu kufanya, na ambacho ni kuokoa maisha tu na si chochote kingine.

Na nimejionea katika hospitali ya Kamal Adwan wiki mbili zilizopita kuna uchungu wa mateso ya watu kwenye wodi ya watoto ilikuwa ni jambo ambalo halipaswi kutokea siku hizi.

Na nadhani hiyo pamoja na siasa, pamoja na msukumo na utetezi kutoka ngazi ya juu, watu kama Rais Biden na timu hii yote ambayo imekuja katika eneo hili kwa suala hili. Na nadhani utambuzi wa jumla kwamba maendeleo hayajafanywa na kwamba tumekuwa tukitoa wito huu kwa muda mrefu.

Na nadhani ni sasa tunaanza kuona kwamba hili likitua ndani ya maeneo mbalimbali ya Israeli, kuelewa kwamba wanapaswa kufanya zaidi na sisi na kuturuhusu kufanya zaidi kwa ajili ya watu wa Gaza, na hawapaswi kuwa na mashaka na kutoaminiana.

Wanapaswa kuelewa kwa nini tuko pale na kile tunachojaribu kufanya na ni kuokoa maisha tu na si kitu kingine chochote.

Hema lililojengwa kwa makopo ya chakula katika makazi ya Deir Al-Balah, Gaza
UN News/Ziad Taleb
Hema lililojengwa kwa makopo ya chakula katika makazi ya Deir Al-Balah, Gaza

UN News:  Na kwa ahadi hizi, ikiwa zote zitatekelezwa, ni changamoto gani nyingine unazohofia, zinazokabili utoaji wa misaada?

Jamie McGoldrick: Kweli, nadhani tunachokabiliana nacho hivi sasa ni hali ambayo ni tete sana na shughuli za kijeshi huko. Mamilioni mengi ya watu wanateseka. Kila mtu katika Ukanda wa Gaza anahitaji aina fulani ya msaada kutoka kwetu.

Na kwa ukweli kwamba suala la sheria na utaratibu ni muhimu huko kwa sababu watu wamekata tamaa sana. Na kwa hiyo wakiona malori, wanakuja na kushambulia malori na kupora na kuchukua vitu.

Na hiyo inamaanisha kuwa baadhi ya chakula hakiwafikii watu wote wanaopaswa kukipata. Na hivyo, ni muhimu kwetu kuweka mambo kwa utulivu. Na jinsi tunavyofanya mambo kuwa shwari ni kufika kila mahali, kujaza mahali hapo na kuhakikisha chakula kila mahali.

Punguza gharama, kuondoa thamani iliyopo. Na ili hilo lifanyike kuwe na utulivu huo serikali inapaswa kuturuhusu kuwe na njia rahisi zaidi ya kutoa msaada.

Kwa sababu hivi sasa upeo wetu wa kupanga ni siku mbili hadi tatu, na tuna hisa ya siku mbili au tatu tu nchini kwa wakati mmoja kwa hivyo lazima tubadilishe hiyo kukosekana kwa utulivu, uvunjaji wa sheria, ombwe la usalama na tuweze kuwa nacho sisi wenyewe kiasi kikubwa cha chakula kinachopatikana kwa sababu tunajua uvamizi wa Rafah unakuja na tunahitaji kuwa na uwezo wa kuweka akiba mapema. Na sasa hivi, hatuwezi kufanya hivyo.

UN News:  Unaposema tunajua kwamba uvamizi wa Rafah unakuja, huna matumaini yoyote kwamba labda hii itaepukwa, kwamba upande wa Israeli umeanza kusikiliza na kujibu vyema shinikizo la dunia?

Jamie McGoldrick: Nadhani wanasikiliza hilo. Lakini nadhani pia wana malengo ya vita, ambayo nadhani yanapinga malengo yoyote ya kibinadamu.

Na nadhani inabidi tuwe katika hali ya kutambua kuwa kwao vita haijaisha, kwao mchezo wa mwisho haujafika. Na nadhani kujitoa Khan Younis ni kuwatayarisha kwa kitakachofuata.

Watoto wakitembea katika mitaa ya Rafah Kusini mwa Gaza
© UNICEF/Eyad El Baba
Watoto wakitembea katika mitaa ya Rafah Kusini mwa Gaza

Na nadhani hicho ni kitu hata idadi ya Waisraeli, ambao wanataka mateka wao warudi, na ni asilimia kubwa miongoni mwao, uchunguzi wowote uliofanywa kwa maoni ya umma wanapendelea sana kumaliza hii hali kupitia Rafah.

Na kwetu sisi hatushiriki sehemu yoyote ya harakati ya kuhamisha watu. Lakini tunapaswa kuwa tayari kwa uwezekano wa watu kuondoka Rafah, kwa sababu kuna maeneo machache sana kwao kwenda. Na tunahaha sana kuweka nyenzo za kutosha, vitu visivyo vya chakula, makazi, vifaa vingine na maji, haswa wakati huu wa mwaka ambapo hali ya hewa inazidi kuwa joto sana na uwezo wa kuwa na msaada wa ulinzi wa huduma za afya za kuhamahama.

Kwa hivyo, mambo hayo yote ni masuala makubwa sana kwetu, na kwa kweli hatuna uwezo na rasilimali hivi sasa. Na hakika tunajitahidi kujiandaa. Kwa hivyo, tunatumai mabomba haya yote yakifunguliwa, fursa hizi zote mpya Kaskazini - tunaweza kuanza kumwaga maji na kufurika mahali hapo kwa kwa msaada wa chakula na vitu vingine, tunajitayarisha kwa lolote litakalofuata.

UN News: Kwa hivyo kimsingi, mnakimbizana na wakati?

Jamie McGoldrick: Haswa, sasa hivi tunaishi katika maisha ya bora mkono wende kinywani. Hatujaweza kushughulikia maswala ambayo yanatukabili. Tunalo bomba fupi tu, tuna hisa ndogo tu, na tuna mahitaji makubwa.

Na bila shaka, hii haijumuishi Kaskazini, ambako hali inatisha zaidi katika suala la mahitaji ya kibinadamu. Hadi tutakapoweza kushughulikia hilo, hatuna nafasi ya kusema kwamba tunaweza kuweka akiba kando kama vile ungefanya katika dharura nyingine, au majanga mengine. Na bado mipango inaendelea kwa uvamizi wa Rafah, ambao unaweza kufurusha hadi watu 800,000.