Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake tunaweza tumedhihirisha katika usanifu majengo India: Rosie na Sridevi

Rosie Paul (kushoto) na Sridevi Changali walianzisha Studio ya Masons Ink mnamo 2013
© Grace Barrett
Rosie Paul (kushoto) na Sridevi Changali walianzisha Studio ya Masons Ink mnamo 2013

Wanawake tunaweza tumedhihirisha katika usanifu majengo India: Rosie na Sridevi

Wanawake

Wakati jukwaa la kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 68 au CSW68 likiendelea hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa likibeba maudhui yanayochagiza usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake leo tunakukutanisha na wanawake wa shoka, maswahiba wawili wahandisi wa usanifu majengo waliodhamiria kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza changamoto ya hewa uka katika sekta ya ujenzi kwa kutumia tofali za matope. 

Rosie Paul na Sridevi Changali kutoka Bangalore, India, nia yao kubwa ni kuusambaza mradi huo nchi zima na hata nje ya India.

Mazingira ya ujenzi yanawajibika kwa karibu asilimia 40 ya uzalishaji wa hewa ukaa duniani. Roise na Sridevi wanasema suluhu iko katika tofali za matope.

Nyumba ya matope ya Thomas Payyapilli ilijengwa kwa gharama ya chini kabisa, na athari ya chini kwa mazingira.
© Grace Barrett
Nyumba ya matope ya Thomas Payyapilli ilijengwa kwa gharama ya chini kabisa, na athari ya chini kwa mazingira.

Safari ya usanifu majengo

Huyo ni Rosie Paul akisema” Siku zote nimekuwa nataka kuinusuru dunia lakini sikuwahi kudhani kwamba usanifu majengo ndio utanisaidia kufanya hivyo..anashirikiana na rafiki yake kipenzi tangu chuo kikuu Sridevi Changali.. anasem aliingia katika tasnia hii akifikiria kuwa kama Indiana Jones kuvinjari ameneo mbalimbali lakini akabaini mtazamo huo hsio hali halisi ilivyo.

Wasanifu majengo hawa ndoto zao ni kujenga majengo endelevu ambayo yanaweza kuhimili dhoruba za tabianchi kama vile mafuriko na joto kali. 

Wakati huo huo, wakichagiza na kushawishi wanawake zaidi kuingia katika tasnia ya usanifu majengo kwa kuwapa mafunzo ya kuwa wajenzi.

Kilichowasukuma kuanzinza mradi huu wa ujenzi wa nyumba za matope kwa mujibu wa Rosie ni changamoto ya mabadiliko ya tabianchi “Sio wasanifu wengi wanaofikiria kuwa mabadiliko ya tabianchi ni jambo ambalo wanahitaji kufikiria, lakini tunajaribu kubadili hilo. Tope kama nyenzo miaka nenda miaka rudi imekuwa ikitumika katika ujenzi, na ni nyenzo safi sana.”

Soundcloud

Matope rahisi kupatikana na gharama nafuu

Kwa Sridevi tope ni lulu na ni kama mazingaombwe kwani nyumba zilizojengwa na matofali ya tope zinaboresha hewa ndani ya nyumba na kuepusha ukungu tofauti na nyumba za sementi na pia zinahifadhi joto zaidi na pia baridi hivyo kuepuka matumuzi ya viyoyozi yanayotumia nishati nyingi ya umeme

“Unaweza kutengeneza matofali ya matope kwa kutumia aina yoyote ya udongo. Tuna udongo mzuri sana mwekundu hapa. Udongo huu unachujwa zaidi. Chembe zote kubwa huondolewa na umechanganyika na uliokuwa mchanga lakini sasa ni vumbi la changarawe. mchanganyiko huu unauongeza maji kidogo sana ili kuulainisha kisha unauwekwa kwenye mashine ya kufyatulia matofali, unachofanya ni kuondoa chembe zote za hewa kutoka kwenye mchanganyiko na kwa hivyo kupata tofanli nzuri sana. Kazi hii ya utengenezaji na uzalishaji matofali hufanywa na jamii za wenyeji hivyo unarejesha riziki, kwenye jamii na athari chanya zaidi kuliko matofali mengine yoyote yanayotumika.”

Kwa miaka mingi kazi ya usanifu majengo  India imekuwa ikifanywa na wanaume hivyo kuwa mwanamke Sridevi anasem ni mtihani hasa unapofanyakazi na wanaume “Mwanzoni wanaweza kukuambia hapana bibiye huwezi kugusa zana, huwezi kupatwa na matope. Lakini hatimaye wanakuacha kwani wanaona hakuja haja ya kuzungumza nawe, kwani utagusa tu hizo zana, na utapata matope. Kwa hivyo hiyo ni njia moja ambayo tumeona ni nzuri ya kukabili kikwazo hicho. Na kisha unahoji ni nani anayepanga majukumu? NUnafanya kile unachojihisi kufanya, kinachokupa furaha. Na kufanya kazi kwa mikono yangu ndicho kinachonipa furaha, kwa hiyo ninafanya hivyo na hii husaidia kujenga uhusiano bora na waashi.

Sindhoor Pangal (kati) alifanya kazi na Masons Ink na timu ya waashi wanawake kuunda nyumba yake ya udongo.
© Sindhoor Pangal
Sindhoor Pangal (kati) alifanya kazi na Masons Ink na timu ya waashi wanawake kuunda nyumba yake ya udongo.

Hakuna kinachomshinda mwanamke akitia nia

Sindhoor Pangal, ni mmiliki wa nyumba awali hakuwa na imani na wanwake hawa wasanifu majengo lakini hatimaye nyumba yake ilijengwa na kampuni ya Rosie na Sridevi  kwa kutumia matofali ya matope baada ya kuelewa kuwa wanawake wanauwezo kama wanaume na wakati mwingine hata zaidi. 

Ujunezi huo kuanzia  i kuanzia wasanifu hadi wajenzi wenyewe wote walikuwa wanawake na anaikubali kazi yao “Ilinichukua muda mrefu ili tu kuwafanya watu waelewe kwamba hatutaki wanaume kwenye mjengo kwa sababu ya dhana kwamba tuko katika majaribio. Unajua wafanyakazi wote ni wanawake. Tunataka kujaribu hii ili kuona endapo inafanya kazi. Wengine walidhani tukianda ujenzi mkuu, basi tutawaleta wanaume hapa. Kwa hivyo nikawaambia wanawake wajenzi sawa, tutaanza kazi na ikiwa kuna kazi yoyote ambayo huwezi kuifanya, njoo uniambie siwezi kufanya hivi, mwanaume anaweza na mimi siwezi, na tutapata mwanaume kuja kuifanya. Na walichukua hiyo kama changamoto.”

Tangu mwaka 2013 Rosie na Sridevi wamekuwa wakifanya kazi hii  na wamepiga hatua lakini Rosie anaamini bado elimu zaidi inahitajika ili watu waelewe vyema uhusiano baina ya nyumba za matofali ya matope na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi “Kwetu sisi ni dhahiri kwamba mabadiliko ya tabianchi huathiri moja kwa moja makazi ambayo utaishi. Na zaidi ni kuhusu majengo. Mafuriko, matetemeko ya ardhi, yote ni kuhusu majengo. Na tunahitaji kuanza kujenga majengo yenye mnepo”.

Ingawa mradi wao unaendelea kupanua wigo lakini bado una safari ndefu kwani ndoto yao ni kufika kila kona ya India na hadi nje ya mipaka ya taifa hilo. 

Lakini kwa sasa wanakila sababu ya kujivunia hasa kwa kuvuja mwisko uliokita mizizi kwa miaka mingi kwamba kuna kazi ambazo wanawake hawaziwezi kwani “Kama mwanamke wengi hawategemei uhamishe milima na pale unapoweza kufanya hivyo basi huzusha mashamsham na kwa kuwa hakuna matarajio ni vyema zaidi.”