Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

CSW

23 MACHI 2022

Katika Jarida la Jumatano Machi 23, 2022 kuna habari kwa ufupi zilkilenga mateso yanawowakibili wanawake wakati wa kujifungua, ujumbe wa Katibu Mkuu katika siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani na wito wa ILO kwa Russia kukomesha uvamizi Ukraine pia  tunaangazia kikao cha 66 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kinachoendelea hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa na hususan hatua zilizopigwa na Tanzania katika kusongesha usawa wa kijinsia, kwenye mashinani tutasikia kuhusu msaada linalotoa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Poland.

Sauti
12'39"

17 Machi 2021

COVID-19 kuingilia huduma za afya kumechangia vifo 239,000 vya kina mama na watoto Asia Kusini:UN 

UNHCR na wadau wa misaada wazindua ombi la dola bilioni 1.2 kusaidi wakimbizi wa Sudan Kusini

Hali ya wanawake ni hali ya demokrasia – Kamala Harris 

Makala imejikita nchini Tanzania na mashinani ni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA

Sauti
12'45"
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akihutubia Kikao cha 65 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW65.
Screengrab from UN Web TV

Hali ya wanawake ni hali ya demokrasia – Kamala Harris 

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akihutubia Kikao cha 65 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW65 mjini New York Marekani, amesema "hali ya wanawake ni hadhi ya demokrasia," akiongeza kwamba Marekani imedhamiria kutekeleza maadili ya kidemokrasia yaliyoko katika Azimio la Ulimwengu haki za binadamu.

Sauti
2'3"

09 MACHI 2020

CSW64 ni fursa ya kuchagiza kasi ya kufikia usawa wa kijinsia, umesema Umoja wa Mataifa. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, baadhi ya wanawake waliopona ugonjwa wa Ebola wametoa shukrani zao kwa mamlaka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema idadi ya watoto waliovuka pori la Darien linalotenganisha Colombia na Amerika ya Kati mwaka 2019 imeongezeka zaidi ya mara saba. 

Sauti
12'30"
UNICEF/Samuel Leadismo

Wanawake nchini Kenya washika hatamu kusongesha amani

Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uwepo wa amani na haki pamoja na taasisi thabiti za kusimamia masuala hayo. Pamoja na hivyo, lengo hilo linasisitiza ushiriki wa jamii nzima katika kutunza na kulinda amani, ikimaanisha pia wanawake ambao ndio waathirika wakubwa pindi amani inapotoweka. Ni kwa kuzingatia hilo sambamba na mazingira tatanishi yaliyotokea nchini Kenya baada ya  uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, wanawake nao wameshika hatamu kusongesha amani.

Sauti
4'29"
UN News/Assumpta Massoi

Sisi ni warendile tutambulike tulivyo: Alice

Yaelezwa kuwa utamaduni ni kielelezo cha ustawi wa kila jamii. Utamaduni hudhihirishwa kwa njia mbalimbali iwe lugha, mila, mavazi, chakula na kadha wa kadha. Kutotambulika kwa utamaduni wa mtu au jamii ina maana ni kutokomea kwa jamii hiyo na ndio maana jamii ya warendile walioko kaunti ya Marsbit nchini Kenya wanapaza sauti ili kabili hilo litambuliwe kwa kina ili hata mila zao basi ambazo si potofu ziweze kutumiwa katika kusongesha maisha si tu kwenye jamii zao bali pia kwingineko ambako zinafaa.

Sauti
3'48"
UN News/Flora Nducha

Ukinzani wa sheria ni kikwazo cha umiliki ardhi miongoni mwa wanawake Tanzania- LANDESA

Mkutano wa 62 wa hali ya wanawake duniani, CSW62 ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini  New York, Marekani, hoja ya umiliki ardhi imetamalaki miongoni mwa washiriki. Wawakilishi wa wanawake na wasichana wa vijijini pamoja na wanawake wenyewe wanabadilishana uzoefu juu ya kile cha kufanya ili kuhakikisha kuwa umiliki wa ardhi unafanyika bila kujali jinsia ya mtu.

Sauti
3'49"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Picha ya UN /Rick Bajornas

Madaraka na usawa vimfikie mwanamke- Guterres

Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Maudhui ya mkutano huo wa wiki mbili ni changamoto na fursa katika kufikia usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake na wasichana waishio vijijini.