Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ProjeKt Inspire: Taasisi inayohamasisha masomo ya STEM nchini Tanzania

Dkt. Lwidiko Edward Mhamilawa, Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya ProjeKt Inspire ya nchini Tanzania katika kuhamasisha masomo ya STEM.
UN News
Dkt. Lwidiko Edward Mhamilawa, Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya ProjeKt Inspire ya nchini Tanzania katika kuhamasisha masomo ya STEM.

ProjeKt Inspire: Taasisi inayohamasisha masomo ya STEM nchini Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ni mwaka mmoja sasa tangu Mkurugenzi Mtendaji  wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women Sima Bahous, akizungumza katika mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW67 alipoeleza kuhusu umaskini wa kidijitali ambao unasababisha kuongezeka kwa pengo la usawa.

"Aina mpya ya umaskini sasa inaikabili dunia, umaskini ambao unawaengua wanawake na wasichana kwa hali inayotia sana uchungu, na umaskini huo ni ule wa kidijitali.  Mgawanyiko wa kidijitali umekuwa taswira mpya ya ukosefu wa usawa wa kijinsia, ambao umesababisha wanawake na wasichana kusukumwa nyuma kama tunavyoshuhudia katika ulimwengu wa leo.” Alisema.

Na sasa CSW ya 68 inatarajiwa kufanyika wiki ijayo kuanzia tarehe 11 hadi 22 mwezi huu huu wa Machi na bila shaka mijadala kuhusu ikiwa hatua zimepigwa au la katika kuelekea kuondoa ule Bi. Bahous aliouita umaskini wa kidijitali.

Linalotia matumaini ni kwamba duniani kote ziko taasisi mbalimbali ambazo zinajitahidi kwa namna mbalimbali kuhakikisha pengo hilo la kidijitali linazibwa.

Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Daktari Lwidiko Edward Mhamilawa, Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi ya ProjeKt Inspire iliyoko nchini Tanzania iliyojikita katika kuhamasisha masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

Daktari Lwidiko ambaye ametembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwanza anaeleza kilichowahamasisha kuanzisha taasisi hii ya ProjeKt Inspire.

Wazo la mwanzo lilianza nauzoefu wetu sisi wenyewe ambao tumeanzisha taasisi hii. Namna elimu sayansi na namna eli kwa ujumla inavyotolewa kwenye nchi. Bada ya kupata kusafiri kidogo na Kwenda nchi nyingine tukaona kuna jambo namna watoto na vijana ambavyo wanajifunza masomo ya sayansi hali ambayo inapelekea watoto na vijana wengi kukimbia hasa watoto wa kike kuyakimbia masomo haya ya sayansi. Kwa hiyo nikasema kwa nini tusifanye jambo tukaanza tu kwa kuzunguka kwenye shule na kuwaambia wanafunzi ,tazama unaweza kuwa daktari unaweza ukawa mhandisi. Tukaona vijana wengi wanaendelea kuvutiwa na jamii inapokea vizuri kwa hiyo tukasema tuendelee. Laki hasa hasa ilikuwa ni kuziba pengo lile ambalo mimi mwenyewe na wenzangu tulikuwa tumepitia katika elimu ya Tanzania tuliona kwamba pengo hilo linahitaji kufungwa ili kuendana na kasi ya karne ya 21.

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wanawake na wasichana katika sayansi, ProjeKt Inspire inaweka msukomo gani?

Sisi tuna manma moja nzuri sana ambayo tunafanya. Tunahakikisha katika miradi yetu yote angalau kunakuwa na wasichana angalau idadi sawasawa na wavulana au zaidi ikiwezekana kwenye ushiriki. Hilo ni la kwanza. Lakini la pili tumeshirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO ofisi ya Tanzania tumeandaa makambi ya sayansi kwa ajili ya kuhamasaisha wasichana ili kuona kwamba masomo ya sayansi yanaweza kuleta mantiki na kuweza kutatua matatizo moja kwa moja kwenye jamii yao. Kwa hiyo hili pengo la usawa lipo lakini mimi niña matumaini. Kuna jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika na serikali, na Umoja wa Mataifa na watu wengine zinaonekana kwamba zinaekekea kuzaa matunda kwa hiyo kuna picha ya matumaini zaidi kwa mabinti kuongezeka kwenye sekta za STEM kuliko ilivyokuwa awali.

Vituo vya sayansi nini?

Kwenye vituo vyetu vya sayansi kuna programu nyingi sana ambazo hawaezi kuzifanya mashuleni kwa mfano kuna kujifunza teknolojia mpya hizo zinazokuja kwa mfano uchapishaji wa 3D, kuna kurusha ndege nyuki, ‘coding’ na uundaji wa programu ambazo ni tekolojia mpya hi zas asa hivi. Lakini pia kujifunza kwa njia ya miradi. Kwenye hivi vituo kuna vielelezo vya sayansi amvayo hata walimu wanakuja kwa ajili ya kujifunza namna gani ya kufundisha sayansi kwa ubora zaidi. Kwa hiyo inakuwa ni chachu ya namna ya kufundisha masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati yanafanyika.

Je, utaratibu wa watu kushiriki katika vituo vya sayansi ni upi?

Vituo kwas asa viko viwili kimoja kiko Dar es Salaam (STEM Park by ProjeKt Inspire Dar es Salaam) maeneo ya Morocco na kingine kiko Tanga (STEM Park by ProjeKt Inspire Tanga) maeneo ya Kisosora.Utaratibu wa kushiriki ziko namna tatu. Moja mtoto mwenyewe anaweza akaja pale na mzazi wake au akaja mwenyewe. Shule pia zinaweza zikaweka miadi kupitia mitandao yetu ya kijamii inatwa ProjeKt Inspire Tz kwenye Intagram au ProjeKt Inspire kwenye X (zamani Twitter). Lakini pia walikuwa wanaweza wakaomba kuja kufanya mafunzo kwenye hivi vituo. Kwa tarifa zaidi mtu anaweza akatembelea kwenye wavuti wetu ambao ni www.projektinspire.co.tz.