Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna pengo la TEHAMA hasa kwa watoto wa kike na wanawake- UN 

Siku ya kimataifa ya wasichana kwenye TEHAMA, Addis Ababa, Ethiopia, 2019.
© ITU/M. Jacobson – Gonzalez
Siku ya kimataifa ya wasichana kwenye TEHAMA, Addis Ababa, Ethiopia, 2019.

Bado kuna pengo la TEHAMA hasa kwa watoto wa kike na wanawake- UN 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Teknolojia za Habari na Mawasiliano au TEHAMA vimekuwa vimekuwa vitu muhimu sana wakati huu wa janga a Corona, au COVID-19 kwa kusaidia kuendelea kuunganisha watu na vile vile kusongesha biashara na hudumu muhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo ambayo ni siku ya wasichana katika TEHAMA. 

Hata hivyo amesema licha ya umuhimmu huo, bado nusu ya wakazi wa dunia hawajauniganishwa kwenye mtandao na wengi wao wanaokosa huduma hiyo ni wanawake na wasichana kwenye nchi zinazoendelea. 

Guterres amesema, “takwimu za hivi karibuni kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano duniani, ITU zinaonesha kuwa pengo la asilimia 17 la matumizi ya intaneti duniani kote. Pengo hilo ni kubwa zaidi katika nchi maskini. Katika maeneo mengine, pengo la ukosefu wa mtandao kijinsia ni kubwa zaidi na hivyo kuongeza ukosefu wa usawa na kuwanyima wanawake na wasichana fursa za kupata elimu, ajira bora na zenye ujira bora na hata kushindwa kufanya biashara.” 

Guterres amesema suala la kila mtu kuweza kupata teknolojia hizo ni jambo muhimu katika kujenga jamii na uchumi na kushughulikia changamoto nyingi zinazokabili dunia hivi sasa. 

Siku ya kimataifa ya wasichana katika TEHAMA inalenga kuchochea harakati za dunia katika kuongeza idadi ya wasichana na wanawake kwenye nyanja ya teknolojia. 

Ni kwa mantiki hiyo Guturres anasema, “hebu leo tuazimie tena kwenye lengo la kuwa na fursa sawa kwa vijana wa kike na watoto wa kike katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati, STEM.”