Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto ukomeshwe kwenye vyombo vya habari na tasnia ya burudani

Kila mwaka, mamilioni ya wasichana na wavulana kote ulimwenguni wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na udhalilishaji.
© UNICEF/Estey
Kila mwaka, mamilioni ya wasichana na wavulana kote ulimwenguni wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na udhalilishaji.

Biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto ukomeshwe kwenye vyombo vya habari na tasnia ya burudani

Wanawake

Hii leo huko jijini Geneva Uswisi mkutano wa 55 wa Baraza La Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeendelea ambapo Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto Mama Fatima Singhateh ametaka kutambulika kwa hatua za mtu mmoja mmoja au za pamoja za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika tasnia ya burudani na vyombo vya habari ili kukomeshwa unyanyasiji huo mara moja.

Katika ripoti yake Singhateh amesema ushahidi unaotolewa na waathirika mashujaa na manusura mara zote umesisitiza hitaji la dharura la kuboreshwa kwa ulinzi wa watoto na vijana katika sekta hii, na kuibua maswali muhimu kuhusu kutotosheleza kwa hatua zilizopo za kuzuia na ulinzi, mifumo ya uwajibikaji na upatikanaji wa haki.

“Idadi kubwa ya kesi za unyanyasaji haziripotiwi, haswa kutokana na mienendo ya nguvu iliyopo, kanuni hatari za kijinsia, hofu ya kulipiza kisasi na kupoteza nafasi za kazi,” mtaalamu huyo alisema. 

Ameongeza kuwa “Mambo haya mara nyingi hujenga mazingira ambayo watu binafsi katika nafasi za mamlaka huwanyanyasa watoto walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na wale wanaotarajiwa kuwa waigizaji na waigizaji.”

Wanaotarajia kuwa waigizaji na waigizaji

Mtaalamu huyo pia ameeleza kugundua kuwa tabia ya unyanyasaji ya kingono, ikiwa ni pamoja na wale wanaoanza kuwafundisha watoto wangali wadogo, ilikubaliwa kama kawaida katika tasnia ya burudani, kwani wahalifu mara nyingi hawakabiliwi na madhara yoyote kwa kutumia mamlaka kinyume cha sheria dhidi ya vijana na wanaotarajia kuwa waigizaji.

“Mazingira ya unyanyasaji wa kazi na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika majukwaa mbalimbali ya burudani hayaelekei tu kuvuka mipaka, lakini pia yanalenga na kuwatumia watoto. Waathiriwa na manusura wamekutana na ukimya, kosefu wa uchunguzi, vitisho au kutokuwepo kwa kuchukuliwa hatua.” 

Mtaalamu huyo akiwasilisha ripoti yake alitoa wito wa kuwepo kwa njia za kupunguza hatari na kuhakikisha kuwa uhusika wa watoto katika tasnia ya burudani, na mienendo ya watu binafsi au biashara ndani ya sekta hiyo, unaendana na sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.