Watoto wangu hawatemewi tena mate, nashukuru UN- Mama Kasereka

Wanufaika wa mfuko wa UN wa kusaidia manusura wa ukatili wa kingono huko Bukavu jimboni Kivu Kusini nchini DRC wakionesha nguo walizotia rangi baada ya mafundisho kutoka shirika linalonufaika na mfuko huo.
UN

Wanawake

“Nilianza kufanya shughuli za kujiuza mwili nikiwa na umri mdogo”, kwa masikitiko makubwa anaanza kueleza ambaye alipoteza wazazi akiwa mdogo na kukulia katika mazingira ya vita nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.

Tweet URL

Masika Kasereka anasema tangu wakati huo hadi wakati ambapo alianza kunufaika na mfuko wa ufadhili wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono, SEA ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2016, maisha yake yalikuwa ya kutangatanga na hata ana watoto wawili ambao kwa miaka yote hiyo hawakuwahi kukanyaga shuleni.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia ufadhili wa mfuko wake huo na mmoja wa wanufaika ni huyu Masika kutoka Bukavu ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini. Yeye ameaanza kuona mwanga katika maisha yake ambayo awali yalikuwa yamegubikwa na kiza kizito, alikuwa kahaba tangu mdogo, yeye akitumia neno kimbaraga kuelezea hiyo shughuli ya kujiuza mwili.

Hatua mpya katika maisha yake ilikuja pale ambapo alikutana na kusaidiwa na shirika la Kavumu chini ya Mama Zawadi Bagaya ambaye anapata ufadhili kupitia mfuko huo wa Umoja wa Mataifa. Amewasaidia wanawake kupata ujuzi mbalimbali ikiwemo ushonaji wa nguo, au Kutur, wakitengeneza nguo za vitenge akitumia neno Tantileri na pia batiki.