Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji Gaza lazima yakomeshwe, Türk aliambia Baraza la Haki za Binadamu

Shule za Gaza zimepigwa au kuharibiwa na makombora tangu mwanzo wa vita.
© UNRWA
Shule za Gaza zimepigwa au kuharibiwa na makombora tangu mwanzo wa vita.

Mauaji Gaza lazima yakomeshwe, Türk aliambia Baraza la Haki za Binadamu

Amani na Usalama

Mauaji yanayoendelea huko Gaza yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 30,000 na lazima yakomeshwe mara moja, mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameliambia Baraza la Haki za Kibinadamu leo mjini Geneva Uswisi, baada ya karibu miezi mitano ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel na kufurusha maelfu ya watu katika eneo hilo, kutokana na kuchochewa na mashambulizi ya Hamas yaliyofanyika Oktoba 7 mwaka jana.

"Vita ya Gaza lazima iishe," Bwana Türk amesema, akisisitiza kwamba "muda umepita sana wa kuleta amani, uwajibikaji na uchunguzi wa ukiukwaji wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu na uhalifu wa kivita unaowezekana kufanywa na pande zote mbili.”

Majinamizi ya vita

"Inaonekana hakuna mipaka  na hakuna maneno ya kuelezea maovu ambayo yanatokea mbele ya macho yetu huko Gaza," Kamishna Mkuu Türk, amesema alipokuwa akiwasilisha ripoti iliyoandaliwa na ofisi yake, OHCHR, juu ya hali ya kukata tamaa katika eneo linalokaliwa la Palestina.

Amesisitiza kuwa kuna "kiwango kisicho na kifani cha mauaji na majeruhi kwa raia katika eneo hilo, na takribani watoto 17,000 sasa wamekuwa mayatima au kutengwa na familia zao.”

Na baada ya kusisitiza kulaani kwake kwa mashambulizi ya ya kushtu yasiyo na uhalali kabisaambayo yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 na 8 Oktoba, mwaka jana pamoja na utekaji wa kutisha na mbaya kabisa wa mateka, Bwana Türk amebainisha kuwa kufikia sasa angalau watu watatu kati ya wanne wa Gaza wameyakimbia makazi yao kutokana na vita, huku kukiwa na "ubomoaji wa kimfumo wa vitongoji vyote ambao umeifanya Gaza kutokuwa na makazi.”

Msichana, ambaye familia yake imekimbia mzozo huo, anasimama nje ya hema lake huko Rafah, Gaza.
© WHO
Msichana, ambaye familia yake imekimbia mzozo huo, anasimama nje ya hema lake huko Rafah, Gaza.

Athari za muda mrefu

Akihutubia Baraza hilo, ambalo ni jukwaa kuu la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa chini ya usimamizi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bwana Türk amesema kuwa maelfu ya tani za mabomu zimeangushwa na Israel kwa jamii kote Gaza tangu tarehe 7 Oktoba.

"Silaha hizi hutuma wimbi kubwa la milipuko ya shinikizo la juu ambalo linaweza kupasuka na kutawanyika pamoja na  kuambatana na milipuko ya kugawanyika, na joto kali ambalo husababisha kuunguza sana na zimetumika katika vitongoji vya makazi yenye watu wengi," amesema mkuu huyo wa haki na kuongeza kuwa "Katika hospitali ya Arish ya Misri, Novemba mwaka jana, niliona watoto ambao nyama yao ilikuwa imechomwa. Sitasahau hili kamwe.”

Raia wako njia panda

Kamishna Mkuu pia amebainisha kwamba uwezekano wa "kulenga kiholela au kupita kiasi unaofanywa na Israeli umesababisha makumi ya maelfu ya watu wa Gaza kutoweka na wanadhaniwa kuwa wamezikwa chini ya vifusi vya nyumba zao”, kabla ya kulaani kurushwa kwa makombora ya kiholela kunakofanywa na makundi ya wapiganaji wa Palestina kote kusini mwa Israeli na hadi Tel Aviv.

Jukumu la msaada

Miongoni mwa nchi 47 wanachama wa Baraza hilo, kumekuwa na uungaji mkono wa karibu wote kwa mkuu wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kulaani mashambulizi dhidi ya jumuiya za Israel yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine yenye silaha ya Palestina, wito wake wa kuachiliwa kwa mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa katika eneo hilo la ulinzi, haja ya usitishaji mapigano mara moja, uwajibikaji kwa ukiukaji wa sheria za vita kutoka pande zote mbili na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.

Kamishna Mkuu Volker Türk awasilisha ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu kwa wajumbe wa kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.
UN News/Anton Uspensky
Kamishna Mkuu Volker Türk awasilisha ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu kwa wajumbe wa kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Msimamo wa Israeli

Kwa Israel, Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa huko Geneva Meirav Eilon Shahar ameshutumu mashambulizi ya kigaidi ya Hamas na kurudia madai yasiyothibitishwa ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na kundi hilo linalojihami.

Akiwa ameketi na mateka wawili walioachiwa huru Aviva Siegel na Raz Ben Ami ambao walishikana mikono kusaidiana wakati wa mjadala, mjumbe huyo wa Israel pia amesisitiza juu ya haki ya nchi yake kujilinda kulingana na sheria za kimataifa za kibinadamu.

"Israel inapigana katika uwanja wa vita ambao Hamas imeunda huko Gaza," amesema akiongeza kuwa "Vita ambayo magaidi hujificha nyuma na ndani ya raia. vita ambayo Umoja wa Mataifa umeshuhudia ikijengwa karibu na chini yao kwa miaka mingi na ikachagua kuipuuza.”

Ameendelea kusema kwamba "Israel imeambiwa mara kwa mara kwamba magaidi ambao wamegeuza misaada, wamejenga vichuguu vya ugaidi, kuua kikatili raia wasio na hatia, kubakwa, kukatwa vichwa, familia zilizochomwa moto wakiwa hai hawawezi kuguswa kwa sababu wanajificha miongoni mwa raia. Hata hivyo, hatuna chaguo. Ni lazima tuwafuate Hamas, la sivyo wataendelea kutufuata.”

Kuonyesha mshikamano

mwakilishi wa Palestina, Ibrahim Khraishi,  amesema, "hakuna mtu anayelaani ukweli kwamba wanawake, watoto na wazee wanauawa Gaza."

Takriban watoto 12,000 na wanawake 8,000 walikuwa miongoni mwa waathirika wa vita, Bwana Khraishi amesisitiza, huku akitaja ripoti ambazo hazijathibitishwa Alhamisi asubuhi kwamba makumi ya Wapalestina wameuawa na jeshi la Israel katika mji wa Gaza wakati wakisubiri malori ya misaada kuwasili.

Mvulana anatazama kitongoji chake kilichoharibiwa na mashambilizi wa makombora huko Gaza.
© UNRWA
Mvulana anatazama kitongoji chake kilichoharibiwa na mashambilizi wa makombora huko Gaza.

“Je, hawa ni wapiganaji, ni ngao za binadamu?" ameuliza, kabla ya kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzuia "mauaji mapya huko Rafah, akimaanisha mashambulizi ya kila upande ya vikosi vya Israel bila kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.”

Mkuu wa haki za Umoja wa Mataifa Türk awali alionya dhidi ya shambulio la ardhini la Israel dhidi ya Rafah ambapo watu milioni 1.5 sasa wanapata hifadhi "licha ya kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu".

Shambulio la Israel "litasababisha hasara kubwa ya maisha, hatari ya ziada ya uhalifu wa ukatili, watu kufurushwa upya hadi eneo lingine lisilo salama na hivyo kutia saini hati ya kifo na kwa matumaini yoyote ya misaada ya kibinadamu yenye ufanisi," amesema Kamishna Mkuu. 

Amemalizia kwa kusema kuwa "Nashindwa kuona jinsi operesheni kama hiyo inavyoweza kuendana na hatua za muda zinazotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki.