Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi: Mayai yangu ni ghali sana kula na hilo ni jambo zuri

Lucette Vognentseva anauza mayai yake mara ne zaidi ya bei ya kuku wa kawaida wa kienyeji
UN News/Daniel Dickinson
Lucette Vognentseva anauza mayai yake mara ne zaidi ya bei ya kuku wa kawaida wa kienyeji

Simulizi: Mayai yangu ni ghali sana kula na hilo ni jambo zuri

Ukuaji wa Kiuchumi

Wafugaji wadogo wa kuku kusini mwa Madagascar wameanzisha mpango wa kukuza kipato chao na kuboresha hifadhi ya mifugo ya kuku wa kienyeji, kutokana na msaada kutoka kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.

Zaidi ya wafugaji 80 wa kuku katika mkoa wa Anosy hadi sasa wamepokea ndege hao wanaoweza kubadilisha maisha, ambao wanatokea India lakini ambao sasa wanastawi nchini Tanzania.

FAO ilileta mayai kutoka nchi hiyo ya Afrika Mashariki ili kuangua vifaranga nchini Madagascar.

Lucette Vognentseva, mmoja wa wamiliki wapya, amezungumza na UN News nyumbani kwake katika mji wa Iftaka.

“Nilipokea kuku watano, wa kike watatu na madume wawili, kutoka FAO Novemba mwaka jana na hadi sasa, kuku wawili kati ya hao wametaga mayai 46. wengine bado hawajataga mayai.”

Hawa ni kuku aina ya Kuroiler na wanafaa kwa kutaga mayai na kwa nyama. Ni bora kuliko kuku wetu wa kienyeji kwa sababu hukua haraka, ni wakubwa, hutoa mayai mengi na hustahimili hali ngumu.

Ninaweza kuuza yai langu moja kwa ariary 2000 sana na dola senti 45 ambayo ni mara nne zaidi ya thamani ya yai la kuku wa kienyeji. 

“Mayai yangu ni ghali sana kula badala yake, watu wanakuja kwangu kununua yai moja ili kuanguliwa kwa matumaini litakuwa dume ambalo wanaweza kulivuka na kuku wao wa kienyeji. Hii itaboresha ufugaji wa kuku wao na itakuwa na faida zaidi kwao.”

Baadhi ya watu wanataka kuleta kuku waoili wapandwe na jogoo wangu, lakini mimi si kukubali kwamba siwezi kuwa na uhakika kwamba kuku wao hawajabeba magonjwa, wangu wamechanjwa kikamilifu na wana afya.

Lucette Vognentseva anamiliki moja ya aina ya kuku wa kienyeji wanaotokana na mayai kutoka Tanzania
UN News/Daniel Dickinson
Lucette Vognentseva anamiliki moja ya aina ya kuku wa kienyeji wanaotokana na mayai kutoka Tanzania

Wanaishi kwenye kibanda nilichojenga na hawazururai kama kuku wa majirani zangu na inabidi ninunue chakula maalum sokoni kwani hawawezi kwenda kutafuta chao.

Ni wanyama wa kufugwa ambao sasa wananitambua. Ninaweza kujua wakati wanahitaji kulishwa au wanataka maji.

Ushauri wangu kwa wakulima wengine wanaofikiria kufuga kuku hawa wa kigeni ni kuwa wajasiri, aina hii safi kutoka Tanzania inatengeneza pesa zaidi. Mpango wangu ni kuongeza ukubwa wa kizazi changu.

Kijijini, watu wamechukua tahadhari na wanakuja kwangu kwa ushauri wa jinsi ya kufuga kuku hawa. 

Nimejulikana kama "mwanamke wa kuku wa kigeni."

FAO inatakiwa kufanya kazi pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP kuboresha lishe katika Ifotaka na kwingineko kwa kuwezesha utoaji wa mayai na nyama kwa mpango wa mlo shuleni kwa watoto unaoendeshwa na WFP.