Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yalaani shambulizi Mashariki mwa DRC ikisema ni "ukatili wa kutisha"

(Picha ya maktaba) Vijana wawili wakiwa wamebeba madumu ya maji baada ya kuteka maji kutoka kituo cha kuteka maji kilichojengwa na UNICEF na wadau wake kwenye kambi ya Bulengo magharibi mwa mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokras…
© UNICEF/UNI418288/Ndebo
(Picha ya maktaba) Vijana wawili wakiwa wamebeba madumu ya maji baada ya kuteka maji kutoka kituo cha kuteka maji kilichojengwa na UNICEF na wadau wake kwenye kambi ya Bulengo magharibi mwa mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

UNICEF yalaani shambulizi Mashariki mwa DRC ikisema ni "ukatili wa kutisha"

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoti (UNICEF) linalaani shambulizi lililoripotiwa kutekelezwa Jumapili kaskazini mashariki mwa Beni karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda. 

Ripoti za awali zinaeleza kuwa idadi ya vifo ni watu 29, wakiwemo watoto wanane kati ya umri wa miaka 4 na 15. 

"Ukatili wa kutisha wa shambulio hilo huwezi kuamini," amesema Mwakilishi wa UNICEF DRC Grant Leaity. "Mashambulizi dhidi ya raia - haswa watoto - yanasababisha mateso makubwa na kudhoofisha muundo wa jamii. Kila mtoto ana haki ya kuishi kwa usalama na usalama, bila hofu ya vurugu na migogoro. 

Matukio ya mauaji, ulemavu na utekaji nyara wa watoto - ambayo yameainishwa na Umoja wa Mataifa kama "ukiukwaji mkubwa" - yameongezeka kwa kasi mwaka huu. Matokeo yake, DRC iko kwenye njia ya kuwa na viwango vya rekodi vya ukiukaji mkubwa uliothibitishwa dhidi ya watoto kwa mwaka wa tatu mfululizo. 

Ongezeko

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kumekuwa na ongezeko la asilimia 41 la idadi ya ukiukaji mkubwa uliothibitishwa dhidi ya watoto katika nusu ya kwanza ya 2023 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita. Kulikuwa na ukiukwaji mkubwa 3,377 dhidi ya watoto 2,420 katika kipindi chote cha mwaka 2022, kulingana na Ripoti ya Katibu Mkuu ya Juni 2023 ya Watoto na Migogoro ya Silaha. 

Iwapo mwenendo huu utaendelea, DRC iko mbioni kufikia viwango vipya tangu Umoja wa Mataifa uanze kufuatilia na kuripoti ukiukaji mkubwa mwaka 2005, na kupita rekodi zilizowekwa mwaka 2022. 

Mashariki mwa DRC imekuwa ikikumbwa na vurugu kwa miaka mingi, lakini migogoro na ghasia zimezidi kuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2022. Zaidi ya watu milioni 6 wanakadiriwa kuhama makwao mashariki mwa DRC, na kufanya hili kuwa janga baya zaidi la wakimbizi barani Afrika na miongoni mwa tatu za juu duniani.