Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN isisubiri siku yake tu ndio ielezee shughuli zake- Wadau DRC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC ilitumia wiki ya Umoja wa Mataifa iliyoenda sambamba na siku ya UN kuonesha kazi za mashirika ya chombo hicho.
UN/Byobe Malenga
Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC ilitumia wiki ya Umoja wa Mataifa iliyoenda sambamba na siku ya UN kuonesha kazi za mashirika ya chombo hicho.

UN isisubiri siku yake tu ndio ielezee shughuli zake- Wadau DRC

Masuala ya UM

Mwaka huu wa 2023, tarehe 24 mwezi Oktoba, Umoja wa Mataifa umetimiza miaka 78 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani.  Chata ya kuanzisha umoja huo unaupatia majukumu makuu manne ambayo ni Kuendeleza amani na usalama duniani, kusongesha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa na kuwa kitovu cha kuratibu vitendo vya mataifa. 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa ulikuwa na siku tano za maadhimisho kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba kwenye mji mkuu, Kinshasa. ukipokea wajumbe mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa katika hafla hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa mikutano wa BOBOTO. 

Kwa siku saba mfululizo sherehe za wiki ya Umoja wa Mataifa nchini DRC zilisheheni  shughuli mbalimbali ikiwemo maonesho ya yale mashirika ya umoja huo yanayofanya shughuli zao nchini humu pamoja na mijadala.. 

Joseph mankamba Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa DRC alisema wiki ya Umoja wa Mataifa ndio mwelekeo ambao tulitaka kutoa kama kikundi cha mawasiliano kwa maadhimisho ya miaka 78 ya Umoja wa Mataifa hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Katika ngazi ya kikundi chetu, tulikubali kupanga shughuli kwa muda wa siku tano za juma ili kuangazia idadi fulani ya mada mulika hatua ya kila siku ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa hivyo, lengo la shughuli hii ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ni kuwasiliana iwezekanavyo kuhusu kile ambacho Umoja wa Mataifa unafanya katika kuunga mkono serikali ya Jamhuri, kupitia mada tofauti, zikiwemo haki za binadamu, amani, utulivu, elimu, afya, misaada ya kibinadamu, masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, mazingira, masuala ya kutokomeza umaskini na mambo mengine yote yanayohusiana na kazi za kila siku za Umoja wa Mataifa.» 

Aidha ameongeza kuwa lengo kuu sio tu kusikiliza raia lakini pia kuwapa nafasi yakujieleza kwakile wanachokijuwa kuhusu kazi za umoja wa mataifa nchini Congo na anamini kuwa hii ninafasi ya ukaribu kati ya raia wa DRC na  Umoja wa Mataifa.

Tweet URL

Baada ya mijadala iliyogubikwa na maswali na majibu kutoka maafisa wa mashirika mbalimbali ya umaoja mataifa na washiriki,wanazuoni walionyesha furaha yao kama anavyosema Francine Makweo kutoka mji mkuu Kinshasa.

“Tunafurahia sana namna ya mawasiliano ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine katika sherehe hizi katika kuboresha maisha ya raia.Kupitia suku hii tumepata nafasi yakujuwa mbinu ambazo Umoja wa Mataifa unatumia ili kuboresha maisha ya raia ndio naweza sema napia mbinu ya taifa yakupambana na kuhamasisha watu ili kupambana na vitendo vya ubakaji na nyanyasaji kwa sababu watu wengi awajui nini ndicho kinaandikiwa katika mpango huo wakitaifa na nimuhimu kwa umoja wamatifa kuhamasisa watu ili wakati unakuwa muanga uweze kujitokeza bila wasiwasi na woga» 

Hornella Mumbella naye pia ni mkazi wa Kinshasa akasema amejifunza kazi za mashirika ya UN kama vile lile la kuhudumia wanawake, UN Women akisema linafanya kazi mwanamke ajitegemee kiuchumi.Na pia majukumu ya mwanamke katika ngazi za uamuzi.

Kulikuwepo pia na maonyesho ya mambo mbalimbali ambayo Umoja wa Mataifa unatekeleza nchini DRC. Stephane Kabanga anadhani kwamba Umoja wa mataifa ni lazima uendeleze kazi hii hasa wakati huu ambapo habari za uzushi zinaandama umoja wa mataifa.

 Ni mpango nzuri na wenye kushukuriwa kwa kuwa nafanya vitu kama hivi ambayo vinawaleta pamoja raia wa DRC na Umoja wa Mataifa.inasaidia kwa raia kuelewa kwa ukaribu nini kila shirika la moja wamataifa inafanya nchini mwao Mipango kama hii lazima ifanyike sio tu katika siku za za kimataifa za umoja wa mataifa lakini pia zinaweza fanyika kila wakati kwa mahali tofauti hasa vijijini ulikuunda ukaribu kati ya jamii na umoja wamatifa hasa katika kipindi hiki ambacho tunapamna dhidi ya taarifa za uhongo ambazo zinaandama UN."

Imeandaliwa na Byobe Malenga, UN News, DRC