Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina mambo mawili ya kusisitiza kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati :Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Nina mambo mawili ya kusisitiza kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati :Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia hali inayoendelea Mashariki ya Kati leo Jumapili amesemaKatika wakati huu wa kushangaza, ambapo Mashariki ya Kati inapokaribia kutumbukia kuzimu ni jukumu langu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoa maombi mawili muhimu ya kibinadamu.

 

Katika tarifa yake iliyotolewa mjini New York Marekani Guterres amesema mosi “Kwa Hamas, mateka lazima waachiliwe mara moja bila masharti.”

Na pili “Kwa Israeli, ufikishaji wa haraka na usio na vikwazo wa msaada wa kibinadamu lazima utolewe kwa vifaa vya kibinadamu na wafanyikazi kwa ajili ya raia huko Gaza.”

Ameongeza kuwa Gaza inakosa maji, umeme na vifaa vingine muhimu. Umoja wa Mataifa una akiba zinazopatikana za chakula, maji, bidhaa zisizo za chakula, vifaa vya matibabu na mafuta, ziko Misri, Jordan, Ukingo wa Magharibi na Israel. Bidhaa hizi zinaweza kutumwa ndani ya masa tu.

Ili kuhakikisha uwasilishaji wa msaada huo, amesema “wafanyikazi wetu waliojitolea katika maeneo hayo, pamoja na washirika wetu wa NGO, wanahitaji kuwa na uwezo wa kuleta vifaa hivi ndani na kote Gaza kwa usalama, na bila kizuizi ili kuuwasilisha kwa wale wanaohitaji.”

Amesisitiza kuwa “Kila moja ya malengo haya mawili ni halali. Hayapaswi kuwa ngao na lazima yatekelezwe kwa sababu ni jambo sahihi kulifanya.”