Machafuko Gaza lazima yakome, watu wanaishi jehanamu wangali duniani:Guterres

20 Mei 2021

Siku kumi zilizopita zimeshuhudia ongezeko  la"hatari na la kutisha" la machafuko na vurugu mbaya zaidi katika eneo linalokaliwa la Wapalestina (OPT), haswa Ukanda wa Gaza, na Israeli, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliambia Baraza Kuu la Umoja huo hii leo.

"Ikiwa kuna kuishi kuzimu hapa duniani, basi ni maisha ya watoto huko Gaza", amesema António Guterre, akielezea kushtushwa sana na kuendfelea kuvurumishwa kwa mabomu ya angani na silaha za kijeshi kunakofanywa na vikosi vya ulinzi vya Israeli huko Gaza ambavyo hadi sasa vimeua zaidi ya Wapalestina 200, wakiwemo watoto 60, na kujeruhi maelfu wengine.
Katibu Mkuu pia ameiita hali inayoendelea kuwa  "Ni vitendo visiyokubalika", maroketi uyasiyochagua yanayorushwa na Hamas kuelekea Israeli ambao wanadhibiti eneo hilo na yanayorushwa na vikundi vingine vya wapiganaji ambavyo vimesababisha vifo vya watu12.

Hali mbaya ya kuhuzunisha

Akitoa wito kwa pande zote kusitisha uhasama, mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa "Mapigano lazima yakomeshwe mara moja".
Ameelezea taswira mbaya ya miundombinu ya raia iliyoharibiwa huko Gaza, njia zilizofungwa, uhaba wa nishati ya umeme unaoathiri usambazaji wa maji, mamia ya majengo na nyumba zilizoharibiwa na kubomolewa, hospitali zilizoharibika na kuwaacha maelfu ya Wapalestina bila makazi.
Ameongeza kuwa "Mapigano yamewalazimisha zaidi ya watu elfu hamsini kuondoka majumbani mwao na kutafuta hifadhi kwenye maeneo yanayosimamiwa na  UNRWA shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina ambayo ni shule, misikiti, na maeneo mengine ambayo hayana maji, chakula, usafi au huduma za afya".
Guterres amesema "amefadhaishwa sana na uharibifu wa vituo vya Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kwamba mitambo ya kibinadamu haipaswi kuvamiwa", ikiwa ni pamoja na wakati wa vita.

Katibu Mkuu António Guterres
UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu António Guterres

Mahitaji ya kibinadamu

Bwana Guterres amesema amekuwa akifanya kazi ya kutoa pesa kutoka kwenye mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF), na mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada wa Umoja wa Mataifa anakusudia kutoa dola milioni $ 14 kutoka kwenye mfuko wa usaidizi wa kibinadamu kwa ajili ya maeneo yanayokaliwa ya Palestina.“Fursa za upataji wa bidhaa za kibinadamu ni jambo muhimu. Mashambulio ya vikundi vya wapiganaji kwenye maeneo ya karibu na maeneo ya kuvuka hayakubaliki ”, ameongeza Katibu Mkuu.
Amesisitiza pia kwamba "ufikiaji wa haraka na bila kizuizi wa misaada ya kibinadamu ni lazima uruhusiwe kuingia Gaza.”

Mtoto akiangalia mtoto mwinzie akiwa amelala darasani kwenye shule inayosimamiwa na UNRWA Gaza
© 2021 UNRWA/Mohamed Hinnawi
Mtoto akiangalia mtoto mwinzie akiwa amelala darasani kwenye shule inayosimamiwa na UNRWA Gaza

Sheria za vita

Kanuni za vita kwanza kabisa zinazingatia ulinzi wa raia amesema Bwana Guterres akihimiza Israeli kutii kanuni za wale wanaosimamia vita na kujizuia kabisa na mashambulizi zaidi katika shughuli zake za kijeshi.
Pia ametoa wito kwa Hamas na vikundi vingine vya wanamgambo kuacha kurusha maroketi kiholela kwa raia wa Israeli kwani ni ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

"Hakuna halalisho lolote kwa pande hizo kinzani katika mzozo kukiuka majukumu yao ya kimataifa", ameongeza mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Akiwa na wasiwasi juu ya mapigano ya ghasia kati ya vikosi vya usalama vya Israeli na Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi uliochukuliwa, Bwana Guterres ameihimiza Israeli "kusitisha bomoabomoa na kufukuzwa watu kwa nguvu katika maeneo yanayokaliwa ya Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki.
"Shughuli zote za ujenzi wa makazi  mapya ni kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa", mekumbusha, na pia akasisitiza kwamba hali katika maeneo matakatifu lazima "yaheshimiwe na kuenziwa.”
 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter