Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto kutoka jamii za asili wako hatarini kwa ajira ya watoto: ILO

Anabisi ni jamii ya kiasili ya warao kwenye kingo za mto Kaituma. kaskazini mwa Guyana.
© IOM Gema Cortes
Anabisi ni jamii ya kiasili ya warao kwenye kingo za mto Kaituma. kaskazini mwa Guyana.

Watoto kutoka jamii za asili wako hatarini kwa ajira ya watoto: ILO

Haki za binadamu

Kutengwa kielimu na kutengwa kwa jamii za kiasili ni sababu zinazochangia Atari ya Watoto kutoka jamii za asili kutumbukizwa katika ajira ya watoto limesema Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, likianisha kwamba wengi wa watoto wadogo hufanya kazi katika kilimo, lakini pia wanapatikana katika kazi za ujenzi, biashara, viwandani na kazi za majumbani.

Haya yapo katika uchambuzi mpya wa ILO, ambao unaonyesha kuwa watoto katika jamii za kiasili wanakabiliwa na hatari kubwa ya ajira ya watoto na mara nyingi hawapati elimu.

Katika nchi zilizofanyiwa utafiti na ripoti kuchapishwa leo , watoto kutoka jamii za asili wana viwango vya chini vya mahudhurio ya shule ikilinganishwa na wengine, haswa wasichana.

Hasara na hatari

Kulingana na matokeo ya utafiti huo, watoto wadogo wa jamii za asili wanakabiliwa na matatizo ya kielimu, ambayo yanawafanya kuwa katika hatari zaidi yakutumbukia kwenye ajira ya watoto.

Wengi wao wanafanya kazi za kilimo, lakini pia wanapatikana katika kazi za ujenzi, biashara, viwanda na kazi za majumbani.

Uchambuzi huo wa ILO unaonyesha tofauti kubwa za kikanda na katika nchi mathalani katika ukanda wa Amerika Kusini mfano chini Peru, utumikishwaji wa watoto miongoni mwa watoto wa jamii za asili ni karibu mara tatu zaidi ya kiwango cha wastani.

Na nchini Ecuado, watoto wa kutoka jamii za asili wana uwezekano wa mara 11.6 zaidi kuhusika katika shughuli hatari ikilinganishwa na wastani wa kitaifa kwa watoto wote.

Watoto wa jamii ya asili ya baré katika kituo cha mafunzo cha kitamaduni huko Puerto Ayacucho, Amazonas, Venezuela.
© UNICEF/Alejandra Pocaterra
Watoto wa jamii ya asili ya baré katika kituo cha mafunzo cha kitamaduni huko Puerto Ayacucho, Amazonas, Venezuela.

Umaskini na unyanyasaji

Kulingana na ILO, utumikishwaji wa watoto miongoni mwa watoto wa jamii za asili ni matokeo ya moja kwa moja ya kutengwa kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ambapo jamii zinateseka.

Shirika hilo limesema na maeneo haya yana uwezekano mara tatu zaidi wa kuwa na umaskini uliokithiri.

Zaidi ya hayo, jamii za asili mara nyingi huwa wahanga wa unyakuzi wa ardhi, hubeba mzigo mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi na migogoro, wana ufikiaji mdogo wa huduma muhimu, na hukutana na vikwazo katika kudumisha njia zao za jadi za maisha.

Kulingana na utafiti huo wa ILO, ukweli huu unaweza kuwalazimisha watoto wa jamii za asili kufanya kazi ili kusaidia familia zao. 

Pia kusababisha matokeo mengine, kama vile unyanyasaji wa wasichana wa jamii za asili na wasafirishaji haramu ambao wanatumia mwanya wa kuvuruga uhusiano wa kifamilia na jamii.

Hakikisho la haki

ILO inatetea kushinda ajira ya watoto na kutengwa kielimu kupitia majibu ambayo yanajumuisha ukuzaji na ulinzi wa haki za watu wa asili kwa upana zaidi.

Hatua hizo ni pamoja na kuzidisha juhudi za kuanzisha mbinu za ushiriki wa watu wa kiasili katika kufanya maamuzi, katika kubuni na kutekeleza sera na programu, katika kupata elimu bora inayostahili kitamaduni na ulinzi wa kijamii, pamoja na kuhakikisha haki ya ardhi.