Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya: Global Youth Forum  na UNIS Nairobi watekeleza mradi wa ‘Football for the Goals’ kwa vitendo

Soka kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu.
UNSOM
Soka kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu.

Kenya: Global Youth Forum  na UNIS Nairobi watekeleza mradi wa ‘Football for the Goals’ kwa vitendo

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Peter Omondi kutoka shirika la vijana la Global Youth Forum nchini Kenya ni mmoja wa vijana ambao mapema mwezi huu kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi waliandaa mechi ya mpira wa miguu iliyohusisha zaidi ya vijana 100 katika Kaunti ya Siaya ili kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Omondi Peter akihojiwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi Kenya anaeleza ushiriki wao katika mradi huu akisema, “kulingana na ripoti, mambo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yanafaa yazingatiwe kila mahali kuhakikisha kila mtu katika ulimwengu anajumuika katika kuendeleza hii miradi ya SDGs.” 

“Huu mradi wa Mpira wa Miguu kwa ajili ya Malengo ,” kijana huyo kutoka shirika la vijana la Global Youth Forum nchini Kenya anaendelea kueleza, “unahakikisha kujumuisha wachezaji wote katika michezo ya mpira, kuwa pamoja, na kuunganisha vijana wote, wazee na akina mama kuja pamoja.” 

Kilichonifurahisha 

Omondi akieleza kitu kilichomfurahisha anasema ni watu kuja pamoja na hii michezo kuandaliwa katika miji iliyoko ndani au pembezoni na hivyo watu wa vijijini kushiriki katika mazungumzo ya Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu. 

“Kama kijana ningependa kuhamasisha vijana wenzangu pale nyumbani na katika maeneo ya ndani kwenye jamii waendelee kujumuika kwa ajili ya SDGs. Hiyo yote itahakikisha kwamba hakuna aliyeachwa nyuma katika haya mazungumzo ya Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.” Anahitimisha kijana Omondi Peter.