Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na Brazil watia saini ushirikiano wa kusongesha SDGs

Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akizungumza na waandishi wa habari katika  Ikulu ya Itamaraty kwenye mji mkuu wa Brazil, Brasilia.
UN Brazil/Isadora Ferreira
Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Itamaraty kwenye mji mkuu wa Brazil, Brasilia.

UN na Brazil watia saini ushirikiano wa kusongesha SDGs

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika siku yake ya kwanza ziarani nchini Brazil, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amepongeza juhudi za serikali za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, na kujadili hatua za kuongeza kiwango cha ufanikishaji wa malengo hayo kwa kuchukua hatua za dharura zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kurekebisha mfumo wa fedha wa kimataifa.

Akizungumza katika mkutano na viongozi waandamizi wa serikali ya Brazil juu ya kuchagiza utekelezaji wa SDGs au Ajenda 2030, Bi. Mohammed amesema “tuko Brazil leo hii kwa sababu hap ani ambako ajenda ya maendeleo endelevu ilizaliwa miaka ya 90 na hatimaye ikawa ajenda ya dunia nzima.”

Naibu Katibu Mkuu akiwa Brazil atatembelea pia eneo la Amazon kwenye msitu mnene ambako anatazamia kuona dira na ahadi za serikali za “kwanza kabisa ya kuona mazingira na hatua kwa tabianchi ni sehemu ya Ajenda 2030.Lakini pia wananchi, watu wa jamii ya asili na watu wote Brazil ni kitovu cha hatua zozote zile na kwa njia moja tunaweza kuhakikisha eneo hilo ni endelevu.”

Wakati wa ziara hii, Mratibu Mkazi wa UN nchini Brazil Silvia Rucks, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira walisaini makubaliano ya ushirikiano ya kuchagiza utekelezaji wa SDGs au Ajenda 2030 nchini Brazil.

Bi. Mohammed amesema utiaji saini huo ni moja yah atua za kuendeleza kuimarisha uhusiano wa kina ba Brazil wa matumaini ya kwamba “sio tu tutafanikisha SDGs, lakini pia tunaweza kusogeza hili katika ushirikiano wa nchi za kusini, na kuona ni kitu gani Brazil inaweza kutoa kama mchango wake duniani.”

Kesho Jumatano, Naibu Katibu Mkuu atatembelea Santarém ambako huko mto Tapajós unakutana na ukanda wa Amazon