Mwaka 2017 joto lilifurutu ada:WMO

18 Januari 2018

Ni dhahiri kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na ongezeko la hewa ukaa yanaendelea, kwani mwaka 2015, 2016 na 2017 imethibitishwa kuwa ni miaka mitatu iliyovunja rekodi ya kuwa na joto la kupindukia katika historia.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya hali ya joto duniani iliyotolewa leo na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO ambalo limesema mwaka 2016 bado unashikilia rekodi ya juu Dunia wakati mwaka 2017 unaoshikilia nafasi ya pili ukiorodheshwa kuwa ni wenye joto la kufurutu ada bila kuwepo na hali ya El Niño, ambayo inaweza kupandisha kiwango cha joto cha mwaka kimataifa.

Tathimini ya kina ya WMO katika vituo vitano vya kimataifa vya ukusanyaji data, imeonyesha kwamba kiwango cha joto duniani mwaka 2017 ni wastani wa nyuzi joto 1.1 kikiwa ni juu ya ilivyokuwa kabla ya maendeleo ya viwanda. Omar Bodoui ni afisa wa WMO anayeratibu masuala ya hali ya hewa ya kila mwaka. Anasema habari sio mwaka gani umeshika nafasi gani katika kiwango cha joto bali ni

(SAUTI YA OMAR BADOUI)

Akiongeza kuhusu hilo Katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas amesisitiza kwamba mwenendo wa muda mrefu wa hali hiyo ndio muhimu na hofu ni kwamba unazidi kuongezeka kwani miaka 17 kati ya 18 iliyovunja rekodi  ya joto la kupindukia yote ipo katika karne hii hali inayotia wasiwasi kuhusu mustakhbali wa dunia.