Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikataba ya kimataifa ya ufadhili wa miradi inayolenga Afrika imeshuka thamani kwa 47%: UNCTAD

Rasilimali fedha na uwekezaji bora ni muhimu ili kufanikisha hatua sahihi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
© Unsplash/Micheile
Rasilimali fedha na uwekezaji bora ni muhimu ili kufanikisha hatua sahihi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Mikataba ya kimataifa ya ufadhili wa miradi inayolenga Afrika imeshuka thamani kwa 47%: UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Matarajio ya uwekezaji wa kimataifa yalionekana ya kusikitisha sana mwaka jana, huku kukiwa na janga la kiafya, mabadiliko ya tabianchi na mshtuko wa kiuchumi na kusababisha kutokuwa na uhakika wa wawekezaji kote ulimwenguni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.

Ripoti hiyo ya” uwekezaji wa kimataifa kwa mwaka 2023” inaonyesha kuwa  “Kupanda kwa kiwango cha mfumuko wa bei, hofu ya mdororo wa uchumi na mtikisiko katika masoko ya fedha vimechangia mipango mingi ya uwekezaji kusitishwa mwanzoni mwa mwaka. Mwishowe, mtiririko wa uwekezaji wa kimataifa umekumbwa na changamoto,ingawa inaonekana kuwa ni thabiti zaidi kuliko ilivyotarajiwa.” 

Wakati uwekezaji wa fecha wa kimataifa wa moja kwa moja FDI ulipungua kwa asilimia 12 mwaka jana hadi dola trilioni  1.3 trilioni, kushuka kulikuwa kwa kiasi kidogo, mtiririko wa uwekezaji kwa nchi zinazoendelea uliongezeka kidogo, na wawekezaji walimaliza mwaka kutangaza miradi mipya katika viwanda na miundombinu.

Afrika uwekezaji ukishuka kwa asilimia 45

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa upende wa Afrika uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje FDI ulishuka hadi dola bilioni 45 mwaka 2022 kutoka dola bilioni 80 mwaka 2021 na ulichangia asilimia 3.5 ya FDI ya kimataifa.

Ripoti ya UNCTAD inasema idadi ya matangazo ya mradi wa greenfield iliongezeka kwa asimilia 39 hadi  kufikia 766. 

Miradi sita kati ya 15 ya juu ya uwekezaji mkubwa wa Greenfild yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 10 iliyotangazwa mwaka 2022 ilikuwa Afrika.

Hali halisi ya kila kanda Afrika

Kwa upande wa Afrika Kaskazini, Misri iliona uwekezaji kutoka nje wa moja kwa FDI ukiongezeka zaidi ya mara mbili hadi kufikia dola bilioni 11 kama matokeo ya kuongezeka kwa ushirikiano wa kuvuka mipaka na kupata mauzo (M&A).

Miradi ya greenfiled iliyotangazwa iliongezeka zaidi ya mara mbili kwa idadi, hadi kufikia 161. 

Mikataba ya kimataifa ya ufadhili wa miradi ilipanda thamani kwa theluthi mbili, hadi dola bilioni 24. 

Mtiririko wa kuelekea Morocco ulipungua kidogo, kwa asilimia 6, hadi dola  bilioni 2.1.

Kwa Afŕika Maghaŕibi, Nigeŕia ilishuhudia uwekezaji wa FDI ukibadilika kuwa hasi hadi punguzo la dola milioni 187 kutokana na kutoweka kwa uwekezaji katika hisa. 

Miradi iliyotangazwa ya greenfield, hata hivyo, ilipanda kwa asilimia 24 hadi kufikia dola bilioni 2. 

Mtiririko wa uwekezaji hadi Senegal ulibakia kuwa dola bilioni 2.6. Mtiririko wa FDI kwenda Ghana ulishuka kwa asilimia 39 hadi  kudikia dola bilioni 1.5.

Afrika Mashariki, ripoti inasema mtiririko wa uwekezaji kwenda Ethiopia ulipungua kwa asilimia 14 hadi dola bilioni 3.7,na  nchi ilisalia kuwa mpokeaji wa pili kwa ukubwa wa uwekezaji wa moja kwa moja toika nje FDI katika bara la Afrika. 

FDI kwenda Uganda ilikua kwa asilimia 39 hadi  kufikia dola bilioni 1.5 hasa kwenye uwekezaji katika tasnia ya uziduaji.

Na ukwekezaji wa moja kwa moja toka nje  FDI kwa Tanzania uliongezeka kwa asilimia 8 hadi dola bilioni 1.1.

Katika eneo la Afrika ya Kati, FDI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ulibakia kuwa dola bilioni 1.8, huku uwekezaji ukiendelezwa Na katika maeneo ya Kusini mwa Afrika, mtiririko ulirudi katika viwango vya awali baada ya kilele cha juu kisicho cha kawaida mnamo 2021 kilichosababishwa na urekebishaji mkubwa wa mashirika nchini Afrika Kusini. 

FDI nchini Afrika Kusini ilikuwa dola bilioni 9  chini ya kiwango cha mwaka 2021 lakini mara mbili ya wastani wa muongo uliopita. 

Mauzo ya mpakani ya M&A nchini humo yalifikia dola bilioni 4.8 kutoka dola milioni 280 mwaka 2021. 

Nchini Zambia, baada ya miaka miwili ya maadili hasi, FDI ilipanda hadi dola milioni 116.