Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA: Mtambo mkubwa zaidi wa nishati ya nyuklia barani Ulaya waunganishwa tena na njia yake ya dharura

Mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhya nchini Ukraine.
Ⓒ IAEA
Mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhya nchini Ukraine.

IAEA: Mtambo mkubwa zaidi wa nishati ya nyuklia barani Ulaya waunganishwa tena na njia yake ya dharura

Amani na Usalama

Baada ya miezi minne, Mtambo wa Nishati ya Nyuklia wa Zaporizhzhya nchini Ukraine (ZNPP) umeunganishwa tena katika njia yake pekee ya dharura.

“Lakini hali ya nishati ya eneo hilo bado ni tete wakati wa mzozo wa kijeshi unaoendelea na sio endelevu.” Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Mariano Grossi ameeleza leo.  

Njia hiyo moja ya umeme ya kilovolti 330 (kV) iliyosalia kati ya njia sita za dharura kabla ya mzozo huo ilikuwa imekatwa tabgu tarehe 1 Machi kutokana na uharibifu uliotokea ng'ambo ya Mto Dnipro. Kazi ya kuunganisha tena njia ya umeme imekuwa ikitatizwa na hali ngumu ya usalama katika eneo la kusini.