Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa shiriki ni neema kwetu na jamii inayotuhifadhi: Wakimbizi Kenya

Serafina, mkimbizi wa Burundi anayeishi katika makazi ya Kalobeyei nchini Kenya, alifungua kibanda cha mboga mwaka 2019 kwa kutumia mkopo wa masharti nafuu kutoka kwa washirika wa sekta binafsi wa UNHCR.
© UNHCR/Pauline Omagwa
Serafina, mkimbizi wa Burundi anayeishi katika makazi ya Kalobeyei nchini Kenya, alifungua kibanda cha mboga mwaka 2019 kwa kutumia mkopo wa masharti nafuu kutoka kwa washirika wa sekta binafsi wa UNHCR.

Mradi wa shiriki ni neema kwetu na jamii inayotuhifadhi: Wakimbizi Kenya

Wahamiaji na Wakimbizi

Serikali ya Kenya inaendesha mradi wa “shiriki” ambao unawapa fursa wakimbizi wanaosihi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini humo kujitegemea kwa kufanya kilimo cha mbogamboga kupitia chama cha ushirika wa wakulima. Serikali hiyo imetenga ekari 21katika kambi ya Kakuma ili kutumika katika mradi huo ambao sio tu unawapa lishe bora wakimbizi, matumaini na kipato lakini pia umekuwa neema kwa jamii za wenyeji.

Katika makazi ya Kalobeyei kambini Kakuma maisha yanaendelea kama kawaida kwa maelfu ya wakimbizi yakighubikwa na pilika nyingi kikiwemo kilimo cha mchicha, Sukuma na mbogamboga zingine chini ya mradi wa shiriki. Abdulazizi Lugazo ni mkimbizi kutoka Somalia na mwenyekiti wa chama hicho cha ushirika wa wakulima anasema, 

Abdulazizi anasema mradi huu ulianza kidogokidogo lakini sasa umepanuka na kujumuisha wakimbizi wengi zaidi, 

Kenya imekuwa mwenyeji wa wakimbizi kwa zaidi ya miaka 30 na inaamini kuwapa fursa hii wakimbizi sio tu inawapa matumaini badi inawajengea uwezo. Mkimbizi kutoka Congo DRC anayeshiriki mradi huu Muhawe Selene ambaye ni mchuuzi wa mbogamboga sokoni anaafiki, 

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mtazamo kama huu wa Kenya unapaswa kuigwa na mataifa mengine kwani unawajumuisha wakimbizi na kusaidia kuleta utangamno baina ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi.

Kwa Abdulazizi mradi huu umemfungulia njia mpya ya matumaini akiwa mbali na nyumbani.

UNHCR Imeishukuru Kenya kwa kuwapa matumaini wakimbizi hawa wakiwa mbali na nyumbani, na Kenya inasema huu ni mwanzo tu kwani iko katika mipango ya kutekeleza sera ambazo ni bunifu na jumuishi zitakazowaruhusu baadhi ya wakimbizi hao nusu milioni na waomba hifadhi nchini humo kufanya kazi na kuishi na Wakenya.