Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa PRM Kakuma wamrejeshea Thowat mwenye miaka 2 utoto wake:UNHCR

Kambi ya wakimbizi ya Kakuma Kaskazini Magharibi mwa Kenyal.
OCHA/Gabriella Waaijman
Kambi ya wakimbizi ya Kakuma Kaskazini Magharibi mwa Kenyal.

Mradi wa PRM Kakuma wamrejeshea Thowat mwenye miaka 2 utoto wake:UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Ulemavu wa aina yoyote ile iwe kwa mtu mzima ama kwa mtoto ni changamoto kubwa , na zaidi ni kwa wtoto ambao mara nyingi ni vigumu kuelewa kwa nini wamezaliwa hivyo. Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya mtoto Thowat mkimbizi toka Sudan Kusini baada ya miaka miwli ya kushindwa kutembea kutokana na ulemavu sasa ana matumaini. Kulikoni ?

Kambini Kakuma kwenye kituo maalumu cha ulemavu wa viungo mtoto Thowat mwenye umri wa miaka miwili akitembea kwa mara ya kwanza kwa msaada wa baiskeli maalumu ya kusukuma yenye magurudumua manne inayomsaidia kwani alizaliwa bila miguu yote.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hivi sasa kwa msaada wa viungo bandia vya miguu, mazoezi maalum na baiskeli ya kusukuma vimemsaidia Thowat kuishi maisha ya kawaida na kufurahia utoto wake ikiwemo kucheza.

Yote haya yamewezekana kutokana na wataalam wenye ujuzi na waliobebea kazi hiyo ambapo mmoja wao ni  Zebidah Monyoncho mmoja wao mtaalam hao na afisa wa tiba ya viungo katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma pia anahusika na masuala ya utu na ujumuishwaji ambapo anasema, “kazi yangu kubwa ni kuhakikisha kwamba watu wanauwezo wa kutembea na kwa hilo ninamaanisha kwamba wanahitaji kuweza kumudu mwendo wao. Hivyo kazi yangu kubwa inajumuisha kuwapa vifaa ili waweze kutembea kwa uhuru.”

Na ndivyo alivyofanya kwa mtoto Thowat ambaye hana lingine la kusema isipokuwa kutoa Shukran na kusema asante.

Mradi huu unafanyika kupitia msaada wa kitengo cha UNHCR cha idadi ya watu, wakimbizi na uhamiaji PRM kinachofadhiliwa na Marekani ambapo Zebidah anasema “mwishoni mwa mwaka 2018 PRM ilisaidia ujenzi wa kituo cha kudumu kambini Kakuma4, na sasa tumehama kutoka kwenye hema na tunatoa huduma zetu kutoka kwenye kituo cha kudumu. Hivyo Shukran zetu za dhati ziende kwa PRM kwa msaada wao.”

Kituo hicho kinatoa msaada kwa wakimbizi na wenyeji, Watoto kwa wakubwa wenye ulemavu na wanaohitaji msaada.