Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Watu wakiona mikoba niliyoshona ni lazima wahoji aliyeshona- Harriet

Ubunifu wa mitindo ya nguo kama hii ya vitambaa vinavyotengenezwa kwa magome ya miti ni moja ya mbinu za kujikwamua kiuchumi
UN News/Matt Wells
Ubunifu wa mitindo ya nguo kama hii ya vitambaa vinavyotengenezwa kwa magome ya miti ni moja ya mbinu za kujikwamua kiuchumi

 Watu wakiona mikoba niliyoshona ni lazima wahoji aliyeshona- Harriet

Ukuaji wa Kiuchumi

Harriet Mkeshimana ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye kwa sasa anaishi katika kambi ya Kakuma katika makazi ya Kalobeyei kaunti ya Turkana nchini Kenya.

Harriet ni mmoja wa wabunifu 200 wanaotengeneza mikoba, vito vya thamani na vikapu. Bidhaa hizo wanazitengeneza kutokana na mali ghafi wanayopata mashinani na ambazo zinalinda mazingira. Soko la bidhaa hizo ni la mashinani na kimataifa.

Wakati Hariet alifika Kenya alikuwa na ujuzi wa kushona akisema kwamba yeye hakumaliza shule na badala yake wazazi walimfundisha ushonaji wa nguo.

(Sauti ya Hariet)

Makazi ya Kalobeyei yametoa fursa kwa Harriet kuimarisha stadi zake za ushonaji na sasa yeye ni mwana mitindo baada ya kuhudhuria mafunzo ya miezi

 kumi katika kituo cha biashara cha Kalobeyei kinachoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataida la kuhudumia wakimbizi, UNCHR pamoja na wadau. Haariet ana ndoto kubwa kwa ajili ya siku za usoni.

(Sauti ya Hariet)

Mfumo wa biashara na vifaa vinavyotumika ukipewa jina la MADE51 unalenga kudumisha utamaduni wa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi na

 kuchagiza ujumuishwaji wa wakimbizi kiuchumi. Aidha mfumo huo wa MADE51 unaoendeshwa na UNHCR kwa ufadhili wa wadau wake unafanikisha ufikiaji wa masoko, ufadhili, uwekezaji na fursa za kiuchumi kwa wote.