Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto, wapaza sauti zao Tanzania wakiadhimisha siku ya kutokomeza ajira kwa watoto

Watoto katika nchi zingine wanajihusisha na aina mbaya zaidi ya ajira kwa watoto. (Maktaba)
© UNICEF/Christine Nesbitt
Watoto katika nchi zingine wanajihusisha na aina mbaya zaidi ya ajira kwa watoto. (Maktaba)

Watoto, wapaza sauti zao Tanzania wakiadhimisha siku ya kutokomeza ajira kwa watoto

Haki za binadamu

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua, Kata ya Gua katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe. 

Kupitia siku hii muhimu kwa Watoto ulimwenguni kote, baadhi ya watoto kutoka Shule ya Msingi Gua wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya, miongoni mwao ni  Lucia Jonas “maadhimisho ha yani muhimu sana kwetu. Naomba serikali na wadau waendelee kutoa elimu kwa jamii ili kukomesha utumikishwaji wa watoto.”

Grace yeye ni muelimishaji jamii kuhusu utumikishwaji wa mtoto kwenye mashamba ya tumbaku, hapa anazungumzia hali ya utumikishwaji ilivyo kwa sasa akisema, “Kulikuwepo utumikishwaji lakini baada ya kutolewa elimu, na elimu inaendelea kutolewa kwas asa sehemu zinazolima tumbaku, ule utumikishwaji haupo na kubwa zaidi tendelee kutoa elimu.” 

Kwa upande wake Innocent David Pesa amewashauri wazazi na walezi juu ya athari za utumikishwaji wa mtoto, “Wazazi na walezi waache kuwatumikisha watoto ili waebde shule kusoma kwani vitendo vya utumikishaji watoto vina madhara kwa watoto.  

Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda Sambamba na kauli mbiu isemayo “Haki za Jamii kwa Wote, Tokomeza utumikishwaji wa Mtoto”