Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chondechonde nchi zote wapokeeni wakimbizi kutoka sudan na msiwarejeshe watokako: UNHCR

Mamia ya wakimbizi wapya wa Sudan wamekusanyika kupokea vifaa vya msaada vya UNHCR katika eneo la Madjigilta katika mkoa wa Ouaddaï nchini Chad.
© UNHCR/Colin Delfosse
Mamia ya wakimbizi wapya wa Sudan wamekusanyika kupokea vifaa vya msaada vya UNHCR katika eneo la Madjigilta katika mkoa wa Ouaddaï nchini Chad.

Chondechonde nchi zote wapokeeni wakimbizi kutoka sudan na msiwarejeshe watokako: UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limezisihi nchi zote duniani kuacha mipaka yao wazi ili kuwapokea wanaokimbia machafuko nchini Sudan na kufuta fikra mbaya ya maamuzi dhidi ya waomba hifadhi.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi shirika hilo likihofia machafuko yanayoendelea nchini Sudan shirika hilo limetoa msimamo mpya kuhusu kurejea Sudan.

Limeshauri kwamba “Watu wanaokimbia mapigano Sudan , pamoja na raia wa Sudan ambao wako nje ya nchi na hawawezi kurejea nyumbani kwa sababu ya vita huenda wakahitaji ulinzi wa kimataifa wa wakimbizi chini ya mkakati wa sheria za kimataifa na za kikanda”

Kwa kuzuka kwa mzozo hapo tarehe 15 Aprili, UNHCR inazitaka nchi zote kuruhusu raia wanaokimbia Sudan, na kusiwe na ubaguzi katika maeneo yao.

“Hii ni kwa ajili ya raia wa Sudan, raia wa kigeni, ikiwa ni pamoja na wakimbizi waliokuwa wakihifadhiwa na Sudan, watu wasio na utaifa, na wale ambao hawana hati za kusafiria au hati nyingine za utambulisho.”

Changamoto za kibinadamu ni lukuki

Tangu kuanza kwa mapigano hayo, UNHCR na washirika wa jumuiya ya ulinzi wa kibinadamu wamekuwa wakiripoti changamoto kubwa za masuala ya kibinadamu na ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kiholela na kusababisha vifo vya raia na majeraha, unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na kuenea kwa uhalifu na uporaji wa miundombinu ya kiraia ikiwa ni pamoja na masoko. , hospitali, majengo, mali za wahudumu wa kibinadamu, na mali za watubinafsi.

Idadi kubwa ya raia wamelazimika kukimbia mapigano, ikiwa ni pamoja na watu ambao tayari walikuwa wakimbizi wa ndani kwa sababu ya migogoro ya awali nchini Sudan, na wakimbizi kutoka nchi nyingine ambao walikuwa wametafuta usalama nchini Sudan.

“Mbali na wakimbizi wapya wa ndani, zaidi ya watu 100,000, wakimbizi wa Sudan na waliorejea, pia wamekimbia Sudan na kukimbilia nchi jirani hasa Chad, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri na Ethiopia," amesema Elizabeth Tan, mkurugenzi wa ulinzi wa kimataifa wa UNHCR akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva hii leo.