Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyama, mayai na maziwa ni virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu: FAO

Ng'ombe wa maziwa ni mali muhimu ya kilimo katika vijiji vya mashinani, ikiashiria utajiri na bima, pamoja na kutoa aina muhimu ya lishe.
© FAO/Lydia Limbe
Ng'ombe wa maziwa ni mali muhimu ya kilimo katika vijiji vya mashinani, ikiashiria utajiri na bima, pamoja na kutoa aina muhimu ya lishe.

Nyama, mayai na maziwa ni virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu: FAO

Afya

Nyama, mayai na maziwa vimeelezwa katika ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kuwa ni chanzo muhimu cha vitutubisho vinavyohitajika mwili ambavyo haviwezi kupatikana kwa urahisi katika lishe itokanayo na mimea.

Ripoti hiyo “Mchango wa chakula cha asili cha wanyama wa nchi kavu kwa lishe bora bora na matokeo yenye afya” iliyotolewa leo mjini Roma Italia inasema hasa katika hatua za awali za maisha kama ya ujauzito na unyonyeshaji, utoto. Umri wa ubarubaru na uzeeni virutubisho vya vyakula hivyo vinahitajika sana.

Thathimini ya kina

Hii ni tathimini ya kwanza ya kina ya FAO iliyoangalia faida na hasara za kula vyakula vitokanavyo na wanayama na inatokana na Ushahidi kutoka kwa nyaraka zaidi ya 500 za kisayansi na sera 250.

FAO inasema sahani ya nyama ya kusindikwa , mayai na glasi ya maziwa pembeni vinaweza kukupa vitutubisho vya msingi kama ptotini, mafuta na wanga na pia vitutubisho vingine ambavyo ni vigumu kupatikana kutoka kwenye mimea kwa ajili ya kiwango na ubora wa lishe inayohitajika mwilini.

Protini yenye ubora wa juu, idadi ya asidi muhimu ya mafuta  pamoja na madini ya chuma, calcium, zinc, selenium, Vitamini B12, choline na madini mengine kama vile carnitine, creatine, taurine hutolewa na vyakula kutoka kwa shambani na wanyama wengine wafugwao, na yana umuhimu na kufanya kazi kubwa za afya na maendeleo ya kimwili.

Kuku ni mali inayoshikiliwa sana kiuchumi na lishe katika afrika ya vijijini na mara nyingi husimamiwa na wanawake.
© FAO/Believe Nyakudjara
Kuku ni mali inayoshikiliwa sana kiuchumi na lishe katika afrika ya vijijini na mara nyingi husimamiwa na wanawake.

FAO imebainisha kuwa madini ya chuma na vitamini A ni kati ya upungufu wa kawaida wa virutubishi kote ulimwenguni, haswa kwa watoto na wanawake wajawazito.

Zaidi ya mtoto mmoja kati ya watoto wawili wa shule ya awali  ambao ni takriban watoto milioni 372 na wanawake bilioni 1.2 walio katika umri wa kuzaa, kulingana na utafiti uliochapishwa katika gazeti la Lancet, wanakabiliwa na ukosefu wa angalau moja ya virutubishi vidogo vitatu ambavyop ni madini ya chuma, vitamini A au zinc.

Robo tatu ya watoto hawa wanaishi Kusini na Mashariki mwa Asia, Pasifiki na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tofauti za kikanda

Haishangazi, kulingana na ripoti hiyo ya FAO kwamba ulaji wa chakula cha wanyama kutoka kwa wanyama hutofautiana sana ulimwenguni kote.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mfano, mtu hutumia wastani wa gramu 160 tu za maziwa kwa mwaka, wakati mkazi wa Maisha ya wastani wa Montenegro, hutumia kilo 338.

Ukiangalia katika suala la mayai, mtu wa Sudan Kusini hutumia gramu 2 kwa wastani kwa mwaka ikilinganishwa na wastani wa kilo 25 kwa mtu wa Hong Kong.

“Mtu wa kawaida nchini Burundi hutumia kilo 3 tu za nyama kwa mwaka, ikilinganishwa na kilo 136 zinazoliwa kwa mtu anayeishi Hong Kong,” limesema shirika la FAO.

Sadio Yalcouyé mtaalamu wa lishe, akitayarisha maziwa ya F-100 na F - 75 kwa watoto wenye utapiamlo (MAS) waliolazwa hospitalini katika Kitengo cha Urejesho na Elimu ya Lishe Bora (URENI) cha hospitali ya Ménaka, Mali.
© UNICEF/N’Daou
Sadio Yalcouyé mtaalamu wa lishe, akitayarisha maziwa ya F-100 na F - 75 kwa watoto wenye utapiamlo (MAS) waliolazwa hospitalini katika Kitengo cha Urejesho na Elimu ya Lishe Bora (URENI) cha hospitali ya Ménaka, Mali.

Nyama na vinywaji kwa ajili ya SDGs

Vikiitumiwa kama sehemu ya mlo ufaao, vyakula vya asili vya wanyama vinaweza kusaidia kufikia malengo ya lishe yaliyoidhinishwa na Baraza la Afya Duniani na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanayohusiana na kupunguza udumavu, vifo miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, uzito mdogo, upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri mdogo, umri wa uzazi, na utipwatipwa na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kwa watu wazima, FAO inaongeza.

Lakini wakati huo huo, sekta ya mifugo "lazima ichangie katika kushughulikia changamoto mbalimbali” amesema naibu mkurugenzi mkuu wa FAO Maria Helena Semedo na mchumi mkuu wa shirika hilo Maximo Torero Cullen katika utangulizi wa ripoti hiyo.

Hatari za mazingira

Bi Semedo ameongeza kuwa "Haya ni pamoja na masuala yanayohusiana na mazingira” kama vile ukataji miti, utoaji wa hewa chafu ya ukaa, maji na matumizi ya ardhi yasiyo endelevu, uchafuzi wa mazingira, na masuala yanayohusiana na afya ya wanyama kama vile magonjwa na ukinzani wa viua viini na masuala yanayohusiana na mifugo kama vile hatari za magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu au zoonotic na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya chakula.

Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.
AMISOM/Omar Abdisalan
Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.

Tahadhari ya nyama nyekundu

Hata hivyo ripoti hiyo inaweka wazi kuwa “ulaji wa hata kiwango kidogo cha nyama nyekundu iliyochakatwa inaweza kuongeza hatari ya vifo na matokeo ya magonjwa sugu, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo na mishipa na saratani ya utumbo mpana.”

Lakini imesema, ulaji wa nyama nyekundu ambayo haijasindikwa kwa kiasi cha wastani huenda ukawa na hatari ndogo, liilisema shirika hilo la FAO na kuongeza kuwa  na inachukuliwa kuwa salama kuhusiana na matokeo ya magonjwa sugu.

Wakati huo huo FAO inasema ushahidi kuhusu uhusiano wowote kati ya maziwa, mayai na ulaji wa kuku kwa watu wazima wenye afya nzuri na magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, kiharusi na shinikizo la damu haujathibitishwa kwa maziwa au sio muhimu kwa mayai na kuku.