Mradi wa WFP waleta neema kwa watoto na wazalishaji wa maziwa Burkina Faso

10 Februari 2020

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP umeleeta neema kwa wafugaji wazalishaji wa maziwa nchini Burkinafaso sio tu kwa kuwaepusha na umasikini lakini pia kukidhi mahitaji ya familia zao na hasa watoto wao wanaopata lishe bora ya maziwa hayo shuleni. 

Katika eneo kame la Dori nchini Burkina Faso miongoni mwa wafugaji walionufaika na mradi wa WFP wa ununuzi wa maziwa ni Aissatou Hama mzalishaji na muuzaji wa maziwa siku yake inaanza kwa kukamua ng’ombe wake kabla ya wanaokusanya maziwa kuwasili kijijini hapo.

Baada ya kukamua anayachuja maziwa yote na kuyajaza katika maguduria tayari kwa kusafirishwa kupelekwa kwenye kituo maalum cha utayarishaji wa maziwa cha WFP , Aissatou Hama anasema

(SAUTI YA AISSATOU HAMA)

Kabla ya mradi wa WFP kufika mambo yalikuwa magumu , tulikuwa tunashindwa kuuza maziwa tunayozalisha, lakini sasa tunaweza kuyauza maziwa hayo kwa urahisi na hili linafaidisha watoto kutoka katika jamii yetu.”

Wanaokusanya maziwa hayo kutoka kwa wafugaji wanayapeleka kwenye kituo cha WFP ambako maziwa hayo yanapimwa kwenye maabara kabla ya kuhifadhiwa katika vyombo maalum ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

Khadijatou Ba ni meneja wa kituo hicho cha WFP kinachokusanya na kununua maziwa.

(SAUTI YA KHADJATOU BA)

Watu katika kijiji hiki waliokuwa wakihamia nchi jirani ya Corte D’voire sasa wamekuwa wakusanyaji wa maziwa. Kupitia mradi huu vijana sasa wamepata ajira katika nchi yao na katika kijiji chao”

Maziwa hayo ni lishe bora kwa watoto wa shule ambao wakati wa kifungua kinywa shuleni wanagawiwa na kutoa asante kwa mradi huo kwani umewafanya sasa waende shule.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter