Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyakula vya mimea vyarejea mezani kwa kasi kubwa, vipi nyama?

Rudi ramos, Mkurugenzi wa mapishi yasiyotumia nyama, Bareburger
UN News/Conor Lennon
Rudi ramos, Mkurugenzi wa mapishi yasiyotumia nyama, Bareburger

Vyakula vya mimea vyarejea mezani kwa kasi kubwa, vipi nyama?

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kwa kipindi cha nusu karne iliyopita, fedha na nyama vimekuwa ni vitu vinaonekana vya kipekee: Duniani kote, kadri utajiri unavyoongezeka hata wa mtu binafsi, vivyo hivyo ulaji wa vyakula vitokanavyo na wanyama.
 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira, UNEP linasema kama kasi ya sasa ya ulaji wa vyakula hivyo utaendelea, basi ifikapo mwaka 2050, mahitaji ya vyakula hivyo itaongezeka kwa asilimia 70.
Hata hivyo jambo ambalo ni saw ana kejeli ni kwamba ongezeko hilo la vyakula vitokanavyo na wanyama halimaanishi limechangia katika kuboresha afya ya binadamu. 

Pamoja na suala kwamba wengi wetu tunakula kiasi kikubwa cha vyakula vya wanyama kuliko kiwango kinachotakiwa kiafya, ufugaji  wa wanyama unachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi, husababisha kutoweka kwa makazi ya viumbe vya dunia, hupunguza bayonuai na unaweza kuchochea maambukizi ya magonjwa yatokayo kwa wanyama kama vile ugonjwa wa Corona au COVID-19

Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.
AMISOM/Omar Abdisalan
Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.

Wapenda ‘Baga’ nao sasa wakubali za mimea

Kuna nuru gizaji hivi sasa, mwelekeo unaweza kubadilika! Unaweza kujiuliza kwa nini? Ni kwa sababu wanasayansi, serikali na hata wapendwa mkate uliotiwa katikati nyama ya ng’ombe kwa kiingereza Burger, sasa wanaanza kutambua faida za milo itokanayo na mimea.

“Mwelekeo wa sasa wa kupenda milo ya mboga mboga utazalisha kiwango kidogo cha hewa chafuzi, utahitaji kiwango kidogo cha maji,” imesema UNEP, ikiungwa mkono na utafiti kutoka Chatham House.

Utafiti unasema mageuzi hayo yanaweza kuachia takribani robo ya eneo la majani ya malisho ya ng’ombe na mifugo mingine kwa ajili ya shughuli nyinginezo. Mlo wenye mimea zaidi unaweza pia kusaidia kupunguza magonjwa sugu kama vile kiharusi, kisukari na saratani, sambamba na gharama zake za matibabu na muda unaopotea wa kazi.

Watu wengi sasa wamekubali changamoto waliyopatiwa, ya kuanza njia mpya za kufurahia vyakula pendwa na kwenda na mabadiliko.

Mkulima wa mboga za majani Mary Kibasa bustanini mwake Dar es salaam, Tanzania.
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu
Mkulima wa mboga za majani Mary Kibasa bustanini mwake Dar es salaam, Tanzania.

Nyama ya mmea au nyama ya mnyama?

Kampuni kama vile Impossible Foods na Beyond Meat ambao walitambuliwa na UNEP mwaka 2018 kama mabingwa wa Mazingira duniani, wanaendeleza soko la vyakula mbadala vitokanavyo na mimea vitakavyotumika badala ya nyama. Nchini Marekani soko la vyakula hivyo limeongezeka kwa kati ya asilimia 29 mwaka 2017 na 2019 na mahitaji ya dunia nayo yanatarajiwa kuongezeka ambapo baadhi ya makadirio yanaonesha kuwa soko lake linaweza kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 74 mwaka 2027.

“Maoni yangu ni wa kwamba nyama itasalia kuwa sehemu ya mustakabali wetu,” anasema Ethan Brown, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Beyond Meat huku akisema swali halisi ni “je itakuwa nyama itokanayo na mimea au nyama ya mnyama?”

Kampuni hizo zinahaha kusaka mbadala wa vyakula ambavyo siyo tu vinaharibu mazingira bali pia ni salama kwa afya ya mlaji kuanzia shambani hadi mezani  ikiwa ni sehemu ya kuelekea mkutano wa viongozi wakuu wa nchi mwezi Septemba mwaka huu wa 2021 ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kumulika mifumo ya chakula ili hatimaye njaa itokomezwe mwaka 2030 huku mazingira yakisalia salama.