Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN ziarani nchini Ukraine

Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi unaruhusu kiasi kikubwa cha mauzo ya chakula cha kibiashara kutoka bandari tatu muhimu za Kiukreni katika Bahari Nyeusi.
UN News
Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi unaruhusu kiasi kikubwa cha mauzo ya chakula cha kibiashara kutoka bandari tatu muhimu za Kiukreni katika Bahari Nyeusi.

Katibu Mkuu wa UN ziarani nchini Ukraine

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasili nchini Poland akiwa njiani kuelekea nchini Ukraine.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wake Stephane Dujarric akiwa Warsaw nchini Poland imeeleza kuwa hapo kesho asubuhi 08 Machi, 2023 Katibu Mkuu Guterres  atakutana na Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky mjini Kyiv kujadili kuendelea kwa njanya zote za Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi katika, pamoja na masuala mengine muhimu.

Hii ni ziara ya tatu ya Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine katika mwaka jana.

Katibu Mkuu Guterres atarejea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani siku ya Alhamisi mchana.

Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi ni mpango jumuishi unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha Mazao na Mbolea yanatoka katika nchi za Ukraine na Urusi mtawalia na kueleka maeneo mbalimbali ya dunia kupitia bahari nyeusi ambapo kwanza mizigo itatua nchini Turkiye kwa ajili ya ukaguzi iwapo mizigo hiyo imebeba silaha  au lah.

Mpango huu umeanzishwa maalum kwakuwa nchi hizo mbili zipo kwenye vita tangu mwezi Februari 2022 hali iliyoathiri soko la dunia kwakuwa nchi hizo zinategemewa kwa uzalishaji wa mazao kama ngano nchini Ukraine na uzalishaji wa mbolea nchini Urusi.