Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njia tano ambazo nyasi za baharini huimarisha bayoanuwai

Seagrass ni moja ya mimea muhimu zaidi ya bahari.
© Unsplash/Benjamin L. Jones
Seagrass ni moja ya mimea muhimu zaidi ya bahari.

Njia tano ambazo nyasi za baharini huimarisha bayoanuwai

Tabianchi na mazingira

Mnamo mwezi Mei 2022, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio namba A/RES/76/265 na kutangaza Machi 1 kila mwaka kuwa Siku ya Nyasi Bahari Duniani.

Nyasi za baharini ni moja ya mifumo ya ikolojia ya baharini iliyoenea zaidi duniani, ikifunika takribani kilomita 300,000 za bahari katika nchi 159.

Ingawa muonekano wa bustani za nyasi baharini unaweza usiwe wa kupendeza kama miamba ya matumbawe au kama misitu ya mikoko, lakini ni maficho ya samaki, hulinda ukanda wa pwani kutokana na dhoruba na ni hifadhi kuu za kaboni, na ni baadhi ya maeneo ya asili yenye thamani zaidi duniani.

Licha ya umuhimu wa nyasi hizo, mifumo hii ya ikolojia iko hatarini.Kwa ulinganifu, ni sawa na kusema uwanja wa mpira wa nyasi baharini hupotea kila baada ya dakika 30 na inakadiriwa 7% ya malisho hupotea ulimwenguni kote kwa mwaka. Asidi ya bahari, maendeleo ya pwani na kupanda kwa joto la bahari kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni vichochezi vikuu vya upotevu wa nyasi baharini.

Tweet URL

Tudumishe siku ya nyasi za baharini

Ili kuongeza ufahamu kuhusu hatari iliyopo kwa mifumo hii ya ikolojia, Umoja wa Mataifa umetenga tarehe 1 Machi kuwa Siku ya Nyasi za Bahari Duniani.

"Mfumo wa ikolojia wa nyasi bahari ni mfano kamili wa hali ya asili inayofanya kazi, ambapo makazi na mtandao maridadi wa maisha umeunganishwa kwa upatanifu kamili," amesema Leticia Carvalho, Mkuu wa Tawi la Bahari na Maji Safi la Kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira UNEP.

"Katika hili, Siku ya Kimataifa ya Nyasi Baharini, hebu tuangazie maajabu ya nyasi za baharini na aina zake, zinavyo na zisivyo fanana na binadamu ambao wanazitegemea," aliongeza Bi Leticia.

Carvalho alisema dunia lazima iweke kipaumbele kwa wakati, kuwe na hatua kabambe na zilizoratibiwa ambazo zinahifadhi, kurejesha na kusimamia kwa uendelevu nyasi za baharini. Hilo linapotokea, nchi zinahitaji kuhakikisha kwamba jumuiya za wenyeji, ambazo zimekuwa zikiishi kwa amani na asili kwa maelfu ya miaka, zinanufaika. Kuongeza juhudi hizi ni muhimu katika kufikia Makubaliano ya Paris na Malengo mengi ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Utunzaji wa nyasi hizi pia unachukuliwa kuwa muhimu katika kusaidia nchi kufikia malengo ya Mfumo wa Bioanuwai wa Ulimwenguni wa Kunming-Montreal, ambao ni mkataba wa kihistoria uliotiwa saini mwaka jana kulinda asili. Mkataba huo ulitiwa saini huku kukiwa na mzozo wa viumbe hai ambao unashuhudia aina za viumbe hai milioni 1 kati ya milioni 8 zikisukumwa kuelekea kutoweka.

Bustani ya nyasi bahari - upanuzi wa kijani kibichi, chipukizi na maua kama nyasi - ni suluhisho bora kwa mabadiliko ya hali ya hewa kwa msingi wa asili.
© Unsplash/Benjamin L. Jones
Bustani ya nyasi bahari - upanuzi wa kijani kibichi, chipukizi na maua kama nyasi - ni suluhisho bora kwa mabadiliko ya hali ya hewa kwa msingi wa asili.

Fahamu mambo 5 kuhusu Nyasi za baharini

Hapa kuna njia tano za kushangaza ambazo nyasi za bahari zinaweza kulinda wanyamapori, kufaidisha watu na kusaidia kuweka msingi kwa siku zijazo endelevu.

1. Nyasi za baharini ni kimbilio la spishi za baharini

Malisho ya nyasi za bahari ni vitalu kwa 20% vya uvuvi mkubwa zaidi duniani, ilipainishwa katika ripoti ya mwaka 2020 kutoka UNEP na wadau wake iliyopewa jina la Out of the Blue: The Value of Seagrass to the Environment and People ikieleza thamani ya Nyasi za Bahari kwa Mazingira na kwa Watu. Kuishi kwa spishi nyingi, kama vile kasa, papa na nguva, hutegemea malisho haya.

Kwa sababu ya mwavuli wake wa chini wa maji wenye majani mengi, nyasi za bahari pia hutoa makao kwa wanyama wengi wadogo wasio na uti wa mgongo, kama vile kaa na uduvi, na pia aina nyingi za mwani na bakteria.

2. Nyasi bahari huchuja maji kwa ajili ya matumbawe, sehemu kuu ya viumbe hai

Mara nyingi huitwa ‘chujio cha maji asilia’, malisho ya nyasi baharini yalielezwa kuwa mfumo bora wa ikolojia katika ripoti ya Out of the Blue. Nyasi hizo zinasaidia maji safi kwa kunasa mchanga wenye kaboni na kunyonya virutubisho na vimelea vya magonjwa. Mifumo inayotawaliwa na nyasi za bahari hutia maji oksijeni kupitia usanisinuru, kuboresha ubora wa maji na kuchochea ukuaji wa matumbawe.

Malisho ya nyasi bahari huunda maeneo yenye bayoanuwai kwa kutoa makazi na virutubisho kwa spishi nyingi.

Kwa sababu ya unyeti wake kwa anuwai ya vifadhaiko na vichafuzi, nyasi bahari ni kiashirio cha mapema cha afya ya kiikolojia ya maeneo ya pwani. Wakati nyasi za baharini zinateseka, hali kadhalika bayoanuai nayo inateseka.

3. Nyasi bahari inasaidia uvuvi na riziki kote ulimwenguni

Nyasi za baharini ni sawa na mimea ya nchi kavu kwa kuwa ina majani, maua, mbegu, mizizi, na tishu zinazounganishwa. Kwa hivyo, ni chanzo muhimu cha chakula cha samaki, pweza, kamba, chaza na na ngisi, ambayo inasimamia uvuvi unaosaidia mamia ya mamilioni ya watu duniani kote, kulingana na ripoti ya Out of the Blue.

Nchini Tanzania, kwa mfano, kupungua kwa nyasi baharini kulionekana kuwa na athari mbaya kwa maisha ya wanawake wanaokusanya wanyama wasio na uti wa mgongo, kama vile konokono wa baharini.

Mallard, au Anas platyrhynchos, bata wa kutisha anayepatikana sana sana katika Hemispheres ya Kaskazini na Kusini. Wanaishi katika maeneo oevu, hula mimea ya maji na wanyama wadogo, na ni wanyama wa kijamii wanaopendelea kukusanyika katika makundi au mif…
Yancheng Broadcasting Television
Mallard, au Anas platyrhynchos, bata wa kutisha anayepatikana sana sana katika Hemispheres ya Kaskazini na Kusini. Wanaishi katika maeneo oevu, hula mimea ya maji na wanyama wadogo, na ni wanyama wa kijamii wanaopendelea kukusanyika katika makundi au mifugo ya ukubwa tofauti. Spishi hii ni babu mkuu wa mifugo mingi ya bata wa nyumbani.

4. Nyasi za baharini ni muhimu kwa spishi zisizo za baharini, pia

Wakati wa kuhama kwao majira ya vuli, bata bukini na bata fulani hula kwenye nyasi za bahari zinazotoka kwenye mchanga wa pwani. Ndege wengine hutafuta wanyama wasio na uti wa mgongo katika maji ya kina kifupi ambayo mara nyingi huzunguka mimea.

Mnamo Desemba 2022, viongozi wa ulimwengu walikubaliana na Mfumo wa Bioanuwai wa Ulimwenguni wa Montreal-Kunming, mkataba ulioundwa kulinda anuwai ya maisha Duniani na kuepusha janga la kutoweka linalokuja. Carvalho alisema kuwa wakati nchi zikiendeleza shabaha zao za kitaifa chini ya mkataba huo, lazima zijumuishe ulinzi wa nyasi za baharini.

"Malisho ya nyasi baharini yanaunga mkono safu ya kushangaza ya maisha na kuyalinda ni muhimu ikiwa tutafikia malengo yetu ya kimataifa juu ya bioanuwai - na lazima," alisema.

5. Nyasi za bahari ni dawa ya mabadiliko ya tabianchi

Mara nyingi hujulikana kama aina ya misitu ya buluu, nyasi za bahari, kama vile zile za nchi kavu, husaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ingawa malisho haya yanafunika asilimia 0.1 pekee ya sakafu ya bahari, ni mifereji ya kaboni yenye ufanisi mkubwa, ikihifadhi hadi 18% ya kaboni ya bahari duniani, ilitaja ripoti ya Out of the Blue.

Nyasi za baharini pia hufanya kama safu ya kwanza ya ulinzi kwenye ukanda wa pwani kwa kupunguza nishati ya mawimbi, kuwalinda watu kutokana na hatari inayoongezeka ya mafuriko na dhoruba.

Kufahamu zaidi kuhusu siku ya nyasi za baharí na taarifa mbalimbali tembelea ukurasa huu kwa lugha ya kiingereza