Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yataka kuundwa njia za ulinzi haraka kuendana na maendeleo ya akili bandia (AI)

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk
UN Photo/Violaine Martin
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk

UN yataka kuundwa njia za ulinzi haraka kuendana na maendeleo ya akili bandia (AI)

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameeleza kusikitishwa sana na uwezekano wa madhara kutokana na maendeleo ya hivi karibuni katika akili bandia (AI)

Kupitia taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Geneva Uswisi Kamishna Turk ameeleza kuwa wakala wa kibinadamu, utu wa binadamu na haki zote za binadamu ziko katika hatari kubwa.

“Huu ni wito wa dharura kwa wafanyabiashara na serikali kuunda njia za ulinzi zinazofaa kwa haraka, njia ambazo zinahitajika kwa haraka sana.”

 Mkuu huyo wa Haki za binadamu amesema ofisi yake inafuatilia suala hilo la akili bandia kwa karibu nawanatoa utaalamu wao wahususi na kuhakikisha mwelekeo wa haki za binadamu unasalia kuwa msingi mkuu wa jinsi maendeleo ya akili bandia yanavyoendelea.