Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwe na enzi mpya ya uadilifu kwenye mitandao ya kijamii ili tukomeshe upotoshaji: Guterres

Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya matamshi ya chuki kwenye Twitter
© Unsplash
Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya matamshi ya chuki kwenye Twitter

Tuwe na enzi mpya ya uadilifu kwenye mitandao ya kijamii ili tukomeshe upotoshaji: Guterres

Haki za binadamu

Nchi lazima zishughulikie “madhara makubwa duniani” yanayosababishwa na kuenea kwa chuki na uongo mtandaoni, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo wakati akizindua ripoti muhimu iliyoundwa ili kuimarisha uadilifu wa habari kwenye majukwaa ya kidijitali.

Kengele ya hayari kuhusu tishio linaloweza kusababishwa na maendeleo yanayokuwa kwa kasi ya Akili Bandia (AI) haipaswi kuficha uharibifu ambao tayari unafanywa na teknolojia za kidijitali zinazowezesha kuenea kwa matamshi ya chuki mtandaoni, pamoja na taarifa potofu na za uongo, alisema.

Muhtasari wa sera ya uadilifu wa habari unasema kunapaswa kuwa na wahusika muhimu katika kuhakikisha usahihi unadumishwa, uthabiti na uaminifu wa taarifa zinazosambazwa na watumiaji.

“Ni matumaini yangu kwamba (sera hii) itatoa kiwango cha dhahabu kwa ajili ya kuongoza hatua ili kuimarisha uadilifu wa taarifa” ameeleza Guterres katika utangulizi.

Kuunganisha na kugawanya

Mifumo ya kidijitali - inayojumuisha mitandao ya kijamii, injini za kutafuta vitu mtandaoni na programu za kutuma ujumbe, zinaunganisha mabilioni ya watu kote duniani, kwa mtandao kama Facebook pekee una watumiaji bilioni tatu.

Mifumo hii imeleta manufaa mengi, kuanzia kwenye kuunga mkono jamii wakati wa shida na mapambano, hadi kusaidia kuhamasisha harakati za kimataifa za haki na usawa wa kijinsia. Pia hutumiwa na Umoja wa Mataifa kushirikisha watu duniani kote katika kutafuta amani, utu na haki za binadamu kwenye sayari yenye afya.

Bado majukwaa haya ya kidijitali yanatumiwa vibaya kupotosha sayansi na kueneza habari potofu na chuki, kuchochea migogoro, kutishia demokrasia na haki za binadamu, na kudhoofisha afya ya umma na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Hatari hizi zimeongezeka zaidi kwa sababu ya maendeleo ya haraka ya teknolojia, kama vile akili bandia,” ameeleza mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa katika ripoti hiyo, akiongeza “imedhihirika kuwa biashara kama kawaida sio chaguo.”

Udanganyifu ni hatari na unaweza leta umauti

Ingawa habari potofu, taarifa za udanganyifu na matamshi ya chuki yanahusiana na kuingiliana, lakini hayo ni matukio tofauti.

Matamshi ya chuki yanarejelea lugha ya matusi au ya vitisho dhidi ya kikundi au mtu, kwa sababu tu ya rangi, dini, kabila, utaifa, au misingi kama hiyo.

Tofauti kati ya taarifa zisizo sahihi na za uongo ni dhamira, ingawa tofauti inaweza kuwa vigumu kuamua. Kwa ujumla, maelezo ya uwongo yanarejelea uenezaji wa taarifa zisizo sahihi bila kukusudia, ilhali taarifa zisizo sahihi sio tu kwamba si sahihi bali zinalenga kudanganya.

Bila kujali, zote zimethibitika kuwa hatari na hata kuua.

“Ingawa vyombo vya habari vya kitamaduni vinasalia kuwa chanzo muhimu cha habari kwa watu wengi katika maeneo yenye migogoro, chuki iliyoenea kwenye majukwaa ya kidijitali pia imezua na kuchochea vurugu,” ripoti hiyo ilisema. "Baadhi ya majukwaa ya kidijitali yamekabiliwa na ukosoaji wa jukumu lao katika migogoro, ikiwa ni pamoja na vita vinavyoendelea nchini Ukraine."

Serikali na wamiliki wa makampuni ya mitandao

Kutokana na tishio hilo, Katibu Mkuu Guterres ametoa wito wa kuratibiwa kwa hatua za kimataifa ili kuifanya anga ya kidijitali kuwa salama na shirikishi zaidi huku pia ikilinda haki za binadamu.

Kumekuwa na kukosekana kwa kiasi kikubwa kwa majibu yenye kujenga. Baadhi ya makampuni ya teknolojia yamefanya juhudi kidogo sana kuzuia majukwaa yao kuchangia kuenea kwa vurugu na chuki, Serikali nazo wakati mwingine zimeamua kuchukua hatua kali - ikiwa ni pamoja na kuzima mtandao na kupiga marufuku, hatua ambazo hazina msingi wowote wa kisheria na kukiuka haki za binadamu.

Wasichana vigori wakitumia simu za rununu na tablet katika kambi ya waki,mbizi ya Za'atari  inayohifadhi wakimbizi wa Syria.
© UNICEF/UN051302/Herwig
Wasichana vigori wakitumia simu za rununu na tablet katika kambi ya waki,mbizi ya Za'atari inayohifadhi wakimbizi wa Syria.

Kanuni ya Maadili

Ripoti inaweka mbele mfumo wa hatua za kimataifa ingawa Kanuni ya maadili ya uadilifu wa habari kwenye mifumo ya kidijitali, ambayo inaangazia njia zinazowezekana wakati wa kulinda haki za uhuru wa kujieleza na habari.

Itajenga kanuni zinazojumuisha kuheshimu haki za binadamu, usaidizi kwa vyombo vya habari huru, kuongezeka kwa uwazi, uwezeshaji wa watumiaji na kuimarisha utafiti na upatikanaji wa takwimu.

Katibu Mkuu Guterres pia ametoa mapendekezo yanayoweza kufahamisha kanuni za Maadili.

Kanuni zinajumuisha wito kwa serikali, kampuni za teknolojia na wadau wengine kuacha kutumia, kuunga mkono, au kukuza taarifa potofu na matamshi ya chuki kwa madhumuni yoyote.

Serikali zinapaswa pia kuhakikisha kunakuwa na vyombo vya habari huru, vinavyoweza kutumika, kwauhuru na viwe vingi, vyenye ulinzi mkali kwa wanahabari wao.

Wakati huo huo, mifumo ya kidijitali inapaswa kuhakikisha usalama na faragha kwa kubuni katika bidhaa zote, pamoja na utumizi thabiti wa sera na rasilimali katika nchi na lugha.

Wadau wote wanapaswa kuchukua hatua za dharura na za haraka ili kuhakikisha maombi yote ya Akili Bandia AI ni salama, yana ulinzi, yanawajibika na yanazingatia maadili, na yanatii wajibu wa haki za binadamu.

Watangazaji na mifumo ya kidijitali wanapaswa kuhakikisha kuwa matangazo hayawekwi karibu na upotoshaji wa mtandaoni au taarifa potofu au matamshi ya chuki, na kwamba matangazo yaliyo na taarifa potofu hayatangazwi.