Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wingi wa wanawake na wasichana katika nyanja ya sayansi ni faida kwa wote: UN

Maria alianza kupenda kujihusisha katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani yalipojitokeza wakati alipojiunga kama mwanafunzi na kampuni iliyokuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kuchora ramani ya vyanzo vya maji baada ya kimbunga Idai kilichopiga baad…
©UNICEF/Madalitso Mvula
Maria alianza kupenda kujihusisha katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani yalipojitokeza wakati alipojiunga kama mwanafunzi na kampuni iliyokuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kuchora ramani ya vyanzo vya maji baada ya kimbunga Idai kilichopiga baadhi ya wilaya kusini mwa Malawi mwaka 2019.

Wingi wa wanawake na wasichana katika nyanja ya sayansi ni faida kwa wote: UN

Wanawake

Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kubwa kwa sekta hiyo na jamii kwa ujumla, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.

Tweet URL

António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 11 amesima siku hii ni ya kutanabaisha hesabu rahisi kabisa kwamba, “Wanawake na wasichana zaidi katika sayansi ni sawa na sayansi bora. Wanawake na wasichana huleta utofauti katika utafiti, kupanua wigo wa kundi la wataalamu wa sayansi, na kutoa mitazamo mipya kwa sayansi na teknolojia, ikinufaisha kila mtu.”

Ujumbe wake umeendelea kueleza kuwa kuna ushahidi unaoongezeka kwamba upendeleo wa kijinsia katika sayansi unasababisha matokeo mabaya zaidi, kuanzia kwenye majaribio ya dawa za ambayo huchukulia mwili wa mwanamke kama wa hali isiyo ya kawaida, kutafuta kanuni zinazoendeleza upendeleo na ubaguzi. 

Hata hivyo Guterres ameongeza kuwa katika maeneo mengi sana duniani, upatikanaji wa elimu kwa wanawake na wasichana ni mdogo au unakataliwa kabisa.  

Wanawake wanapotazamia maendeleo katika taaluma za kisayansi, ukosefu wa usawa na ubaguzi unaendelea kuzuia uwezo wao. 

Kana kwamba hiyo haitoshi ameongeza kuwa “Wanawake ni chini ya theluthi moja ya wafanyikazi katika sekta ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu na kidogo zaidi katika nyanja za kisasa. Mtaalamu mmoja tu kati ya watano wanaofanya kazi kwenye akili bandia ni mwanamke. Ni lazima na tunaweza kufanya juhudi zaidi kuchagiza wanasayansi wanawake na wasichana kupitia ufadhili, mafunzo kwa vitendo na program za mafunzo ambazo zinatoa jukwaa la kufanikiwa.” 

Msichana akifanya jaribio la kisayansi la kemia katika shule ya sekondari mjini Lusaka, Zambia.
© UNICEF/Karin Schermbrucker
Msichana akifanya jaribio la kisayansi la kemia katika shule ya sekondari mjini Lusaka, Zambia.

Katibu Mkuu amehitimisha ujumbe wake akisema kupitia mfumo maalum, vivutio vya kuwafanya wabaki, na programu za ushauri ambazo huwasaidia wanawake kushinda vikwazo vilivyopo na kujenga taaluma vitasaidia sana. 

Na muhimu zaidi, ameongeza ni kwa kusisitiza haki za wanawake na kuvunja mila potofu, upendeleo, na vizuizi vya kimuundo. 

Na wito wake ni kwamba “Sote tunaweza kufanya sehemu yetu kuibua talanta kubwa sana ya ulimwengu ambayo haijatumiwa tukianza na kujaza madarasa, maabara na vyumba vya bodi na wanasayansi wanawake.”