Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yapitisha bajeti ya $3.4 trilioni kwa 2023

Bendera za mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa zikipepea nje ya makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani
UN Photo/Rick Bajornas
Bendera za mataifa mbalimbali wanachama wa Umoja wa Mataifa zikipepea nje ya makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani

UN yapitisha bajeti ya $3.4 trilioni kwa 2023

Masuala ya UM



Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa hii jioni limepitisha bajeti ya dola bilioni 3.4 kwa ajili ya shughuli za Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa 2023.

Bajeti hiyo (Dola za Kimarekani $3,396,308,300) imepitishwa na Baraza Kuu bila kupitia kura baada ya kuidhinishwa na Kamati ya Tano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Utawala na Bajeti.


Baraza Kuu limepitisha mpango unaopanua hatua katika maeneo kama vile maendeleo, haki za binadamu na misaada ya kibinadamu.


"Ninawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Tano, mwenyekiti na wajumbe wa ofisi na sekretarieti kwa kuhakikisha kwamba shirika letu linafadhiliwa vya kutosha ili kukabiliana na matatizo mengi yanayoikabili dunia." Rais wa Baraza Kuu, Csaba Kőrösi, alisema kupitia ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter.


Tukuo hili lilitegenewa kufanyika wiki moja nyuma hadi Ijyumaa hii ya terehe 30 Desemba ambapo Kamati ya Tano ilipomaliza kikao chake kikuu kuipa UN bajeti ya 2023.


Bajeti hiyo mpya ni ya nne tangu kuanza kwa mzunguko wa kila mwaka ulioanza mwaka wa 2019. Wasilisho liliwasilishwa na Katibu Mkuu António Guterres Oktoba mwaka jana 2021.
Bajeti hiyo inapanua hatua katika eneo la maendeleo, kwa kuimarisha shughuli za Unctad, Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi wa Kawaida na Shirika la Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Makazi ya Watu, UN-Habitat.