Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nakipenda Kiswahili, nilikisoma na sasa nakifundisha:Mwalimu Clemence Mukamuhoza

Bi. Clemence Mukamuhoze, Mwalimu wa Kiswahili akisimama mbele ya Shule ya Sekondari ya Kanisa Katoliki ya GS Butare katika Wilaya ya Huye katika Mkoa wa Kusini mwa Rwanda.
Picha: Clemence Mukamuhoze
Bi. Clemence Mukamuhoze, Mwalimu wa Kiswahili akisimama mbele ya Shule ya Sekondari ya Kanisa Katoliki ya GS Butare katika Wilaya ya Huye katika Mkoa wa Kusini mwa Rwanda.

Nakipenda Kiswahili, nilikisoma na sasa nakifundisha:Mwalimu Clemence Mukamuhoza

Utamaduni na Elimu

Lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha adhimu na kubwa barani Afrika na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi elimu na utamaduni UNESCO kinazungumza na watu zaidi ya milioni 200 duniani na kwasababu ya umuhimu na mchango wake ndio maana shirika hilo likatenga siku maalum ya kuiadhimisha lugha hiyo kila mwaka Julai 7.

Sasa lugha hiyo imeendelea kupanua wigo na kukumbatiwa katika nchi mbalimbali hata zile ambazo awali haikuwa lugha ya taifa na sasa imefanywa kuwa lugha ya taifa na miongoni mwa lugha za kufundishia mashuleni kuanzia ngazi ya chekechea hadi chou kikuu mfano Rwanda.   

Miongoni mwa mashuhudua wa kukua kwa lugha hiyo ni mwalimu Clemence Mukamuhoza ambaye anafundisha Kiswahili katika shule ya sekondari ya Kikatoliki ya GS Butare wilayani Huye kwenye jimbo la Kusini la Rwanda na anaeleza ilikuwaje hata akakijua Kiswahili “Nilipofika kidato cha tatu nilimkuta mwalimu anafundisha Kiswahili nah apo nikapenda lugha hiyo  na kuwa nah amu ya kuijua zaidi, na niliposhinda mtihani wa taifa niliendelea kwenye shule nyingine ambayo wanajifunza mkono wa lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kinyarwanda na kutokana na kuipenda lugha yhiyo nikachagua Kiswahili.” 

Anasema kwa kuwa lugha hiyo sio rahisi sana ilibidi akaze mkanda kuimudu 

” Hapo ndio nilitia bidi sana , nikajua misamiati mingi, nilifanya utafiti katika vitabu tofauti ili nijue Kiswahili zaidi kwa kuwa nilikuwa ninakipenda sana. Na baada yah apo kufika kidato cha sita nilifaulu ten ana nikachaguliwa kuelekea chou kikuu ambako pia nilisoma Kiswahili chou kikuu cha Rwanda tawi la Rukala.”  

Uchache wa waalimu wa Kiswahili ulinifanya nijikite na lugha hii 

Alipohitimu stashahada yake ya kwanza ya lugha Bi. Clemence alianza kutafuta kazi ya ualimu na kwa mujibu wa lugha alizosomea angeweza kufundisha Kiingereza, Kiswahili na Kinyarwanda lakini akaamua kujikita na Kiswahili kwa nini? “Kutokana na kuwa waalimu wa Kiswahili ni wachache kila mahali nilipoenda wananichagua niwe mwalimu wa Kiswahili.” 

Hivi sasa Clemence anafundisha Kiswahili katika shule hiyo ya GS Butare kuanzia kitado cha pili hadi cha sit ana kuna hamasa kubwa miongoni mwa wanafunzi kujifunza lugha hii “Wapo wengi sana wanaotaka kujua Kiswahili wan hamu ya kujua kuna tofauti gani kati ya Kiswahili na lugha nyingine na wakikutana njiani na watu wanaongea Kiswahili wanapenda sana kwani Kiswahili ni lugha zuri sana Nina wanafunzi kama 2050 na tuko wawili wawili.” 

Rwanda ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitumia lugha ya Kifaransa, Kinyarwana na Kiingereza kwa nini wanafunzi wanaona umuhimu wa kuikumbatia lugha ya Kiswahili hivi sasa: “Niliwauliza wanafunzi siku moja kuhusu hilo wakasema kuna nchi jirani kama Tanzania wana lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa , tukienda huko lazima tuzungumze Kiswahili na Kenya na mahali popote wanapotaka Kwenda Afrika Mashariki kwa kuwa wanatumia lugha ya Kiswahili.” 

Kiswahili kuwa lugha ya kimaifa kuna tija gani Rwanda 

Kwa sasa hivi lugha ya Kiswahili imekuwa bidhaa ya kimataifa baada ya kutangazwa na UNESCO mwaka jana kama lugha ya kimataifa na kutengewa siku maalum ya kuiadhimisha lugha hiyo je hii imeleta hamasa Rwanda ya kujifunza lugha hii? “Ndio kwa kuwa ninapowafundisha wanasema wanalipenda sana somo hili na wanataka kusoma lugha hiyo hasa ukizingatia kwamba ni lugha mpya ambayo haijasambaa sana Rwanda.” 

Rwanda hivi sasa imekuchukua Kiswahili kama lugha ya taifa na kimeanza kufundishwa kuanzia ngazi ya chini ya watoto wa elimu ya chekechea hadi chou kikuu kitu ambacho mwalimu Clemence anasema kimemchagiza kuikumbatia zaidi lugha hii. “ Nilifurahi niliposikia matangazo hayo nikasema ni vizuri sana kwani lugha ya Kiswahili naipenda na watu wanaipenda ukilinganisha na lugha nyingine na ukilinganisha na zamani ambapo ilikuwa haijulikani sana.” 

 

Bi. Clemence Mukamuhoze (kulia), mwalimu ambaye anafundisha Kiswahili katika shule ya sekondari ya Kikatoliki ya GS Butare wilayani Huye kwenye jimbo la Kusini la Rwanda akihojiwa na Flora Nducha
Picha: UN News
Bi. Clemence Mukamuhoze (kulia), mwalimu ambaye anafundisha Kiswahili katika shule ya sekondari ya Kikatoliki ya GS Butare wilayani Huye kwenye jimbo la Kusini la Rwanda akihojiwa na Flora Nducha

Changamoto ya lugha ya Kiswahili Rwanda 

Kwa mujibu wa mwalimu Clemence ingawa lugha hii inapendwa sana na inazidi kupanua wigo Rwanda kuna changamoto ya walimu “Kwa mfano katika shule yangu tuko wawilimu wawili tuu ambao tunafundisha kifdato cha kwanza hadi cha sita takriban watoto 250 ni wengi, lakini kwa kuwa tunaipenda lugha hiyo hatuna uchovu wowote kwani polepole ndio mwendo hapa nchini Rwanda itawezekana punde si punde.” 

Mwisho kabisa mwalimu Clemence anapenda kuto wito kwa wanafunzi wote kuhusu lugha ya Kiswahili ambayo sasa imekuwa bidhaa ya kimataifa “Ninawashauri watie bidi na kusoma sana lugha hii ya Kiswahili na kuifanyia utafiti kwa kuwa ni muhimu sana kwao na kwa nchi yetu ya Rwanda. Kwa mfano tukipata walimu wengi kila shule inaweza kuwa na waalimu zaidi ya wawili au watatu na kila mtu anaweza kujua Kiswahili kutokana na kuwa wanafunzi wengi watasoma somo hilo.”