Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukiadhimisha siku ya lugha ya mama tuhakikishe ujumuishi wake shuleni na katika jamii:UNESCO

Mazingira mazuri shuleni huleta tabasamu kwa wanafunzi.
UNHCR/Catherine Wachiaya
Mazingira mazuri shuleni huleta tabasamu kwa wanafunzi.

Tukiadhimisha siku ya lugha ya mama tuhakikishe ujumuishi wake shuleni na katika jamii:UNESCO

Utamaduni na Elimu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limehimiza watu kila mahali kukumbatia utofauti uliopo duniani kwa kuunga mkono lugha mbalimbali mashuleni na katika maisha ya kila siku.

Kaulimbiu ya siku ya mwaka huu ni “kukumbatia lugha mbalimbali kwa ajili ya ujumuishi katika elimu na jamii”, na siku hii huadhimishwa kila mwaka Februari 21.

Maadhimisho haya lengo lake ni kuenzi utofauti wa lugha mbalimbali ambapo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema lugha hizi “Ni urithi wa binadamu ambao thamani yake haipimiki”

Akizungumzia maudhui yam waka huu Bi. Azoulay amesema “Ni muhimu sana kwa sababu wakati asilimia 40 ya wakazi wa dunia hawana fursa ya elimu kwa lugha zao wanaoziongea na kuzielewa , inazuia upatajai wao elimu lakini pia fursa zao za urithi na utamaduni wao.”

Ameongeza kuwa mwaka huu umuhimu mkubwa umeelekezwa katika ulimu kwa lugha mbalimbali kuanzia utotoni ili kwa watoto , lugha yao ya mama iwe siku zote iwe na thamani kwao.