Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP27 ikielekea ukingoni Guterres atawaka washiriki kusimama kidete na kutimiza ahadi

Skrini ya jumla ya COP27 inaonyesha logan rasmi ya Urais wa Misri: "Pamoja kwa Utekelezaji".
UNIC Tokyo/Momoko Sato
Skrini ya jumla ya COP27 inaonyesha logan rasmi ya Urais wa Misri: "Pamoja kwa Utekelezaji".

COP27 ikielekea ukingoni Guterres atawaka washiriki kusimama kidete na kutimiza ahadi

Tabianchi na mazingira

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 umepangwa kufunga pazia katika muda wa saa 24 zijazo, lakini nchi zimesalia kugawanyika katika masuala kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na hasara na uharibifu unaosababishwa na zahma hiyo ya kimataifa,  amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuzitaka pande zote kuchukua hatua za haraka na kutimiza ahadi dhidi ya changamoto kubwa zaidi inayowakabili wanadamu. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Sharm El Sheikh nchini Misri António Guterres amesema "Ni wazi kuna kuvunjika kwa uaminifu kati ya Kaskazini na Kusini, na kati ya nchi zilizoendelea na zinazoibukia kiuchumi. Huu sio wakati wa kunyoosheana vidole. Mchezo wa lawama ni kichocheo cha uharibifu unaohakikishiwa pande zote mbili,"  

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameitaka nchi kutoka aina ya hatua za maana ambazo watu, na sayari wanazihitaji sana. "Ulimwengu unatazama na una ujumbe rahisi, simameni na mtimize," amesisitiza Katibu Mkuu. 

Hatua juu ya hasara na uharibifu 

Bwana. Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia kwamba uzalishaji wa hewa chafuzi duniani uko katika viwango vya juu zaidi katika historia, na athari za mabadiliko ya tanianchi zinadidimiza uchumi na jamii. 

"Njia ya ufanisi zaidi ya kujenga upya uaminifu ni kwa kutafuta makubaliano kabambe na ya kuaminika juu ya hasara na uharibifu na usaidizi wa kifedha kwa nchi zinazoendelea. Wakati wa kuzungumza juu ya hasara na uharibifu wa fedha umekwisha. Tunahitaji hatua,” amesema,Katibu Mkuu akiwataka wafanya mazungumzo kutoka na suluhisho madhubuti juu ya moja ya maswala ambayo ni mwiba kwenye meza ya COP ya mwaka huu, au mkutano wa wanachama, wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi. 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia amewataka wajumbe wa mazumajadiliano hayo kutoa ishara za wazi kwamba sauti za wale walio mstari wa mbele kwenye kupambana na mgogoro huo zinasikika, huku kuungua na kuzama majini kukiwa mbele ya macho yao. 

Amewahiza “Kuakisi udharura, kiwango na ukubwa wa changamoto inayokabili nchi zinazoendelea. Hatuwezi kuendelea kukataa haki ya mabadiliko ya tabianchi kwa wale ambao wamechangia kidogo katika mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na wanaumia zaidi.” 

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano ya mabadiliko ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa, suala la hasara na uharibifu limejumuishwa katika ajenda rasmi. 

Kuundwa kwa kituo kipya cha kifedha ili kufidia hasara iliyokabiliwa na nchi zilizo hatarini zilizoathiriwa zaidi na majanga ya asili, ni hitaji kuu la kitengo cha mazungumzo kinachojulikana kama Kundi la 77, ambalo linawakilisha karibu nchi zote zinazoendelea. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza katika mshikamano wa COP27 na Rais wa COP27, Sameh Shoukry, aliyesimama kulia.
UNIC Tokyo/Momoko Sato
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza katika mshikamano wa COP27 na Rais wa COP27, Sameh Shoukry, aliyesimama kulia.

Nishati jadidifu njia ya kuepuka kuzimu 

Katibu Mkuu pia amegusia suala jingine ambalo limewasumbua wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi katika siku zilizopita, la kuweka azma ya kuzuia ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzi joto 1.5. 

"Lengo la kuhakikisha joto linasalia nyuzi joto 1.5 sio tu suala la kuweka lengo kuwa hai ni suala la kuwaweka watu hai. Ninaona nia ya kutimiza lengo la kusalia katika juzi joto 1.5 lakini lazima tuhakikishe kwamba kujitolea kunaonekana katika matokeo ya COP27," amesema Guterres akiongeza kuwa upanuzi wa makampuni ya mafuta kisukuku ni "kuteka nyara ubinadamu”. 

Kwa mara nyingine Katibu Mkuu ametoa hoja kwa ajili ya nishati jadidifu, na mkataba wa mshikamano wa mabadiliko ya tabianchi duniani na akitaka nchi zilizoendelea kuongoza katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. 

"Mkataba na nchi zilizoendelea kuongoza katika kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi. Na mkataba wa kuhamasisha pamoja na taasisi za fedha za kimataifa na sekta binafsi ,msaada wa kifedha na kiufundi kwa nchi zinazoibukia kiuchumi ili kuharakisha hatua za mpito kuelekea kwenye nishati mbadala". 

Bwana Guterres amesisitiza kwamba nishati jadidifu nini njia ya kutoka kwenye barabara kuu ya Kwenda kuzimu, akikumbusha moja ya ujumbe wenye nguvu kutoka kwenye hotuba yake wiki iliyopita katika ufunguzi wa COP27. 

Kutoa fedha zinazohitajika 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ameomba kutmizwa kwa ahadi ya dola bilioni 100 kila mwaka katika ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi ahadi iliyotolewa kwenye mkutano wa COP15 huko Copenhagen. 

Amezitaka nchi wanachama kuchukua hatua kwa makubaliano ya kuongeza uwekezaji wao mara mbili katika kujenga mnepo na kurekebisha benki za maendeleo za kimataifa na taasisi za fedha za kimataifa. 

"Lazima watoe msaada ambao nchi zinazoendelea zinahitaji ili kuanza kuhamia kwenye nishati mbadala na njia zenye mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi", amesisitiza. 

Saa zinayoyoma 

Hatimaye, Bw. Guterres amewakumbusha washiriki wa mazungumzo hayo kwamba saa za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi zinayoyoma na kwamba wana nafasi ya kuleta mabadiliko, hivyo lazima wachukue hatua haraka. 

"Tumekubaliana suluhu mbele yetuya  kukabiliana na hasara na uharibifu, kuziba pengo la utoaji wa hewa chafu, na kutoa fedha", amehitimisha bwana Guterres. 

Leo Alhamisi asubuhi, rasimu ya uamuzi wa mwisho, au taarifa ya hitimisho ilichapishwa na Urais wa COP27.  

Hata hivyo, wataalam wa mashirika yasiyo ya kiserikali au NGO wamesema nyaraka hiyo ya kurasa 20 bado ni orodha tu ya chaguzi ambazo lazima zihaririwe. 

Nyaraka ya sasa inaangazia lengo la nyuzi joto 1.5 na kurejelea sayansi, ikikariri wito wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Glasgow wa kupunguza makaa ya mawe lakini haitaji mafuta na gesi.  

Pia nyaraka inarejelea mara mbili kuhusu fedha za ufadhili na kujenga mnepo na inakaribisha kipengee cha ajenda kuhusu hasara na uharibifu, lakini haihitaji wito wa kuanzishwa kwa kituo kipya cha kifedha. 

Odudu-Abasi James Asuquo, mwanaharakati wa vijana kutoka Nigeria katika mkutano wa COP27 huko Sharm El-Sheikh, Misri.
UN News/Laura Quinones
Odudu-Abasi James Asuquo, mwanaharakati wa vijana kutoka Nigeria katika mkutano wa COP27 huko Sharm El-Sheikh, Misri.

Mjadala wa watu 

Leo, mamia ya wawakilishi wa mashirika ya kiraia wamekitumia kikao cha COP27 kudai haki ya mabadiliko ya tabianchi, wakigusia hatua zile zile ambazo Katibu Mkuu alizitaja baadaye katika mkutano wake na waandishi wa habari. 

Sherehe ilianza kwa baraka kutoka kwa watu wa kiasili wa Brazili, zikionyesha jukumu muhimu la imani kama sehemu ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. 

"Sote tumeunganishwa, wanadamu na wasio wanadamu, kila kitu ni kitakatifu na kilichoundwa hakiwezi kuwa sehemu ya soko. Maliasili ni uhai,” amesema mkuu wa kikundi hicho. 

Mkutano huo ulioitwa “Mjadala wa Watu”, ambao hufanyika kila mwaka katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, mwaka huu umeshirikisha wawakilishi wa jamii za watu wa asili, wanawake, vijana na wafanyakazi, miongoni mwa wengine. 

Mmoja baada ya mwingine, wanaharakati wameshiriki maono na uzoefu wao kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na wamezungumza kuhusu haki za binadamu ambazo, wamesisitiza, zinakiukwa na mgogoro wa sasa wa mabadiliko ya tabianchi. 

"Vijana wa kipekee kutoka Kaskazini na Kusini mwa dunia wamesimama pamoja kwa mshikamano wakiomba hatua zichukuliewe. Lakini tunahitaji kutafuta zaidi ya matumaini. Tunahitaji walio mamlakani kusikiliza na kutekeleza suluhu,” amesema mmoja wa viongozi wa wawakilishi wa vijana. 

Huku zikiwa zimesalia chini ya saa 36 katika mazungumzo katika COP27, wanaharakati wanadai hatua dhidi ya hasara na uharibifu.
UN News/Laura Quinones
Huku zikiwa zimesalia chini ya saa 36 katika mazungumzo katika COP27, wanaharakati wanadai hatua dhidi ya hasara na uharibifu.

Maandamano kwa ajili ya haki 

Baada ya kukutana kwenye mkutano huo, washiriki wote walitoka na kufanya maandamano mafupi kwenye eneo la nje la kituo cha mikutano cha kimataifa cha Sharm el-Sheikh yaliyomalizika kwa kukaa ndani, ambako walisoma azimio la watu wa COP27 kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi. 

Nyaraka iliyoidhinishwa na mashirika kadhaa yaliyopo, inataka "Mabadiliko ya mfumo ili kuhakikisha na kuwezesha mabadiliko ya haki kwa asilimia 100 ya mifumo ya nishati mbadala inayomilikiwa na watu, ulipaji wa madeni mabadiliko ya tabianchi kwa kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo 2030 na kushughulikia changamoto zilizopo za muda mrefu na uharibifu, kuondolewa kwa nishati ya mafuta kisukuku, na kuhakikisha mazingira salama na wezeshi kwa mashirika ya kiraia.” 

Ina Maria Shikongo, mwanaharakati kutoka jamii za asili nchini Namibia, ameiambia UN News kuwa "Niko hapa kwa sababu nina hasira. Jamii zangu tayari zimeathiriwa na ukame unaoendelea kwa muongo mmoja uliopita. Watu wangu hawajaona mvua kwa miaka kumi iliyopita. Maisha yao yanaathiriwa tayari,"  

Bi. Shikongo amesema kuwa Namibia kwa sasa ni moja ya nchi kame zaidi Kusini mwa Afrika na bado viongozi wa kimataifa wanajadili iwapo wanapaswa kulipa hasara na uharibifu. 

Amesisitiza kuwa "Serikali zetu zinaendelea kukopa fedha ili tu ziweze kusaidia jamii wakati sisi ndio tunawajibika kwa shida ya mabadiliko ya tabianchi. Namibia ni shimo la hewa ukaa, hivyo hiyo ina maana kwamba Kaskazini mwa dunia, wana deni kwetu kutulipa fidia kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi.” 

Reply

Reply all

Forward